Dalton Elijah
JF-Expert Member
- Jul 19, 2022
- 968
- 1,978
"Tumeenda Ikulu baada ya uchaguzi wa mwaka 2019 na 2020, kwa kauli ya Rais mwenyewe amesema yaliyojitokeza 2019 na 2020 hayatajirudia tena. Tumeshiriki kikao, Mwenyekiti Mbowe anatuongoza, tulikuwa na Mnyika na Kinana alikuwa anaongoza timu ya CCM na nyaraka tunazo, wakasema yaliyojitokeza hayatajitokeza tena, hiyo ni kauli ya Kinana na ipo kwenye maandishi. Nini kilichojitokeza 2024? Tumesimamisha wagombea 88 Tarime wamekata karibia asilimia 60 kabla hatujaingia kwenye uchaguzi, vitongoji 500 wamekata asilimia 60.
Kwa mujibu wa waziri wa Tamisemi alisema wagombea 12600 wa upinzani wamekatwa kwasababu mbalimbali ikiwemo kukosea kujaza fomu, kugonga miuri vibaya na kadhalika, maana yake tunaenda kwenye uchaguzi CCM ikiwa tayari imeshinda viti zaidi ya 2000 na kwa mujibu wa takwimu zetu wagombea zaidi ya 60,000 waliondolewa.
Kuna wanachadema wanaweza kusimama na kusema kwamba tukienda kwenye uchaguzi kwa mazingira haya tunaweza kushinda? Yupo?anyooshe mkono hapa aseme mimi mkiniacha hivi na jimbo langu nitashinda.
Tusidanganyane, tumekaa vikao tukathibitisha bila kuwa kuacha shaka kuwa mazingira ya sasa hatuwezi kushinda lazima tutafute mbinu za kukabiliana na hawa watu ili tuende kwenye uchaguzi ambao ni huru na haki. Sasa mtu anasimama anasema ooh sijui msipoenda kwenye uchaguzi chama kitashindwa, hii si sehemu ya biashara, kama unataka kufanya biashara kafungue duka ufanye biashara. Hii ni taasisi ya kisiasa ya mapambano na tutashinda."- John Heche, Makamu mwenyekiti wa Chadema bara, akizungumza na watia nia ya ubunge 2025Anaye