John Heche asimamia semina elekezi Karatu, ukumbi wazidiwa na umati

Mimi najiuliza, kwa nini huwa kunakipindi semina hizi na mikutano ya ndani huwa inapigwa marufuku na viongozi wake kukamatwa na Wakati mwingine inafanyika tena kwa Amani kabisa?

Inapokuwa imekubalika kufanyika polisi huwa hawana maelekezooo!! Au? Anayejua hili atujuze

Hongereni Chadema kwa mutano huo
 
Sasa mbona mnalialia kwamba mnanyimwa nafasi za kujumuika?

Ebu acheni uongo basi!

Hilo la kunyimwa kukutana wala halina mjadala, na ushahidi upo. Nakumbuka zamani nikiwa mdogo nililelewa na mama wa kambo, mbali ya kunitesa sana, pia alikuwa na tabia ya kuninyima chakula. Sio kwamba alikuwa hanipi kabisa maana ningekufa, ila anaweza kunipa mara moja kwa siku, tena sio cha kushiba. Nikawa nashitaki kwa baba yangu hali hiyo. Akawa akimuona baba yangu akawa ananijazia chakula kisha anamwabia baba yangu, mtoto wako si huwa anakuambia simpi chakula, hicho hapo ni nini? Huyo John Heche kuwepo hapo kwenye mkutano, haimaanishi kuwa cdm hawakataliwi kufanya mikutano yao, tena kwa kakatazo haramu.
 
Swadakta
 

Hilo huwa linafanyika kama mbinu ya kuwadiscourage cdm ili watu wakate tamaa kuwaunga mkono. Hizi ni mbinu zilizokuwa zinatumika huko nchi za ulaya mashariki na vyama tawala vikongwe kama ccm, ili kubaki madarakani dhidi ya wapinzani wao. Pia ni mbinu chafu za nchi nyingi zinazotawaliwa na madictator. Na iwapo cdm itaonyesha kupata bado uungwaji mkono kuelekeo uchaguzi, lazima zitatumika tena mbinu nyingine ovu kuzuia huo uungwaji mkono. Hayo mambo hayafanyiki bahati mbaya, bali ni calculated.
 
Unateseka sana na vipicha vya mwaka 2015 ili iweje?
Hii picha haiwezi kuwa ya 2015. Hiyo t-shirt aliyova Heche, zilianza kuvaliwa mwaka Jana kwenye uchanguzi wa ndani wa CDM Taifa. Wanawake wamevalia vitenge vilivyoanza kuvaliwa 8/3/2020 siku ya wanawake. Hii ni picha ya mwaka huu bila shaka yoyote.
 
Vipi corona imeisha? Mbona sioni barakoa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…