- Source #1
- View Source #1
Baada ya ukimya wa muda mrefu na msimamo wa kutoshiriki uchaguzi bila marekebisho ya kisiasa, hatimaye mwanasiasa John Heche ameonesha mwelekeo mpya. Kupitia mahojiano maalum, Heche amekiri kuwa harakati za “No Reform No Election” zimepoteza mwelekeo na hazina maana tena katika hali ya sasa ya kisiasa.
Amesema yuko tayari kushiriki uchaguzi ujao, akisisitiza kuwa ni muhimu kujipanga ndani ya mfumo uliopo ili kuleta mabadiliko ya kweli.
🎧 Sikiliza mahojiano kamili hapa
Amesema yuko tayari kushiriki uchaguzi ujao, akisisitiza kuwa ni muhimu kujipanga ndani ya mfumo uliopo ili kuleta mabadiliko ya kweli.
🎧 Sikiliza mahojiano kamili hapa
- Tunachokijua
- Chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA kuelekea uchaguzi mkuu 2025 kimekuwa kikiendesha ajenda inayojulikana kama 'No reforms, No election' yenye lengo la kuhamasisha na kuchochea kufanyika kwa mabadiliko ya mifumo ya uchaguzi ili kuwezesha uchaguzi huru na wenye haki ili kuepusha malalamiko yaliyotokana na mapungufu yaliyojitokeza katika chaguzi zilizopita. Kupitia ajenda hiyo mara kwa mara, chama hicho kimekuwa kikisisitiza kuwa bila mabadiliko hakutakuwa na uchaguzi.
Madai
Julai 8, 2025 kumeibuka kipande cha video katika mitandao mbalimbali ya kijamii kinachomuonesha Makamu Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) akizungumza kuwa hoja ya No reforms No election haina chochote na haiwezi kuendelea.
Uhalisia wa taarifa hiyo
JamiiCheck imefuatilia na kujiridhisha kuwa kipande hicho cha video kimehaririwa kutoka kwenye video halisi ili kupotosha uhalisia.
Julai 08, 2025 kituo cha televisheni cha St. Bongo walichapisha video za mahojiano waliyoyafanya na Heche katika mtandao wao wa Youtube. Tazama hapa na hapa kuona video hizo.
JamiiCheck imerejelea video hizo na kubaini kuwa John Heche alizungumzia mambo mbalimbali ikiwemo hali ya kisiasa nchini pamoja na msimamo wao kuhusu mabadiliko wanayoyataka kwenye mifumo ya uchaguzi ili waweze kushiriki uchaguzi mkuu ujao.
Kipande cha video kilichohaririwa kimetoka katika mahojiano hayo yaliyochapishwa na kituo hiko hiko ili kupotosha uhalisia na kubadili maana iliyokusudiwa.
Sehemu ya kipande ambacho kinasikika Heche akisema; “Hoja ya No reforms No election haina mashiko, haiwezi kuendelea, haina chochote cha maana” kimehaririwa kutoka kwenye maneno;
“Mwenyekiti wetu aliwekwa ndani wakitegemea chama kita “freeze” watu watakaa ndani. Sasa baada ya Mwenyekiti kukaa ndani, mi nikaendelea na ziara na ikawa kubwa zaidi ndiyo wakaja ni ile ya Mchome, hatutambui uongozi tukaja na solution. Wakaja na hii ya Said Issa, kwahiyo haya yote ni mambo ambayo malengo yake ‘Ultmate’ ni kuzuia no reforms no election wala hii kesi haina mashiko haiwezi kuendelea, haina chochote cha maana. Lakini lengo kubwa ni kuzuia kwa muda hoja ya No refoms no election”. John Heche, Makamu Mwenyekiti CHADEMA