John Heche: CHADEMA itatoa taarifa ya michango yote, baada ya tarehe 29 ya Kamati kuu

John Heche: CHADEMA itatoa taarifa ya michango yote, baada ya tarehe 29 ya Kamati kuu

Mafyangula

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2025
Posts
557
Reaction score
1,039
Makam Mwenyekiti wa CHadema John Heche wakati akijibu moja ya swali aliloulizwa kupitia kipindi cha Jana na Leo kuhusu kampeni ya Tone Tone hadi sasa CHadema wamekusanya kiasi gani amesema bado yeye ajui hii ni kutokana na kufungiwa kufanya shughuli zozote zile za kichama.

Soma Pia: John Mnyika: Zuio la Mahakama halijatufanya CHADEMA tusitishe Michango ya Tone Tone

Ila amesema miongoni mwa mambo ya kwanza kufanya baada ya tarehe 29 ya Kamati kuu ni kuwatangazia Watanzania ni kiasi gani wamechangia chama, kiasi gani zipo na zitakwenda wapi.

 
Asante Mafyangula kwa kutuletea updates hizi muhimu! Ni jambo la kutia moyo sana kusikia kuwa CHADEMA wamejipanga kutoa taarifa kamili ya michango yote ya Tone Tone baada ya Kamati Kuu. Uwazi na uwajibikaji ni nguzo muhimu sana katika uendeshaji wa chama, na ni haki yetu sote kama wanachama na wapenzi wa demokrasia kujua jinsi michango yetu inavyotumika.

Tunasubiri kwa hamu taarifa hiyo, naamini itajibu maswali mengi na kuimarisha imani. Ni hatua nzuri sana kuelekea uwazi zaidi!
 
Back
Top Bottom