John Heche: CHADEMA siyo Chama cha Fujo, wanaotishia kuua Watu ni CCM, Polisi hawachukui hatua

John Heche: CHADEMA siyo Chama cha Fujo, wanaotishia kuua Watu ni CCM, Polisi hawachukui hatua

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, John Heche, amesisitiza kuwa chama chake hakiamini katika vurugu bali kinafuata njia za kidemokrasia kupata uongozi. Akizungumza Juni 17, 2026 kwenye mahojiano na East Africa Radio, Heche ameeleza kuwa CHADEMA imevumilia uonevu mkubwa, ikiwemo viongozi wao kutekwa na kuuawa, lakini bado wanasimamia amani na hawajawahi kufanya mafunzo yoyote ya siri ya kiuhalifu.

Heche amefafanua kuwa maandamano ni haki ya kikatiba na kisheria, na CHADEMA inayafanya kwa kufuata utaratibu na kutoa taarifa rasmi. Ameshutumu baadhi ya makundi kama UVCCM kwa kutoa kauli za vitisho vya kuua na kuteka watu, huku akishangaa kuona vyombo vya dola vikiwanyamazia wanaotoa matamshi hayo na badala yake kuwasingizia wapinzani kuwa ni wafanya fujo.

Pia Heche amevitaka vyombo vya habari nchini kuacha uoga wa kuogopa kukosa teuzi na badala yake vianike ukweli kuhusu matukio ya utekaji wa raia. Akitolea mfano utekaji wa makada kama Mdude na Mwenyekiti wa Vijana Iringa, Ibrahim Mvovera, akisisitiza kuwa wanaoteka na kutishia maisha ya watu ndio wanaovuruga amani ya nchi na si CHADEMA.

 
Back
Top Bottom