Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tanzania Bara John Heche ametoa wito kwa wafuasi wa chama hicho na Watanzania kwa ujumla wake kuungana pamoja katika kuhakikisha wanapigania haki zitakazopelekea kutatua matatizo aliyodai kuwa yanaipeleka nchi pabaya endapo hatua stahiki za kushughulikia hazitachukuliwa
Akizungumza na Wanahabari kwenye viunga vya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam leo, Jumanne Julai 15.2025 Heche amedai kuwa matatizo ya Tanzania yapo kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo katika mihimili mitatu ya dola yaani Serikali, Bunge na Mahakama
"Watanzania popote mlipo mchukue hatua, hatuwezi kuendelea hivi tena kwa sababu watu wataumia kwa muda mrefu sana.., leo ni siku ya 97 Mwenyekiti wetu (Tundu Lissu, Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa) yuko ndani kwa kesi ambayo wao ndio walioifungua, wao ndio wanapaswa kuwa na ushahidi"