PreGE2025 John Heche: Kikatiba bado Chadema ina nafasi ya kushiriki Uchaguzi mkuu 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, John Heche, anasema chama hicho bado kina nafasi ya kushiriki kwenye uchaguzi mkuu wa 2025, na kwamba kutosaini kanuni za maadili hakuwaondoi kikatiba kushiriki uchaguzi, kwani hakuna muda wa mwisho wa kusaini — wanaweza kufanya hivyo siku yoyote watakayotaka.

Aidha, Heche amesisitiza kuwa msimamo wa CHADEMA mpaka sasa ni "NO REFORMS NO ELECTION".

Kikatiba mbunge anatakiwa awe mwanachama wa siasa. Wabunge 19 wamefukuzwa na chama chao kwa hiyo kupoteza sifa za kuwa wabunge. Mwezi wa 6 wanamaliza ngwe yao kama wawakilishi wa chama chao wanaotambuliwa na Bunge.
Matamko kama haya ndio yanaonyesha kuwa hamna Plan B. Kwa kusema aliyosema ni kuwa wanaamini kuwa ukarabati wa Katiba na taratibu za uchaguzi utafanyika kabla ya Bunge kuvunjwa. Hawako serious.

Amandla...
 
Wewe hujajifunza 2019, 2020 na 2024? Unataka wakagombee huku wakiwa na matumaini tu ya kupata chochote? Watu wameuwawa na kuumizwa kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa, unategemea ninj kwenye uchaguzi mkuu? Wawape viti vya ubunge mkawasumbue bungeni?
 
Ambao hamjajifunza ni nyie. Mnataka kushindana kwenye sprints wakati mashindano ni ya marathon.
Hivi mnataka kutuaminisha kuwa hayo mnayohofia yanatokea wakati wa uchaguzi tu? Na kuwa mkizuia uchaguzi ndio hayatawapata?

Kwanini upoteze nguvu huku unajua 100% uchaguzi unaenda kuibwa?
 
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Heche, amedai kwamba chama chake bado kina nafasi ya kushiriki katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu endapo madai yake ya kutaka mabadiliko katika mfumo wa uchaguzi nchini yatafanyika kabla ya uchaguzi huo.

Imeandikwa na Azam Media
 
nijuavyo mimi kuna wakati vyama vya siasa vinasaini kanuni za maadili ambazo ndio zimesainiwa juzi na vyama 18 isipokuwa CDM na wakati wa uteuzi wa wagombea ndio kila mgombea anasaini fomu na. 10 ya kuheshimu maadili kwa hiyo hapa naona Heche anachanganya
 
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, John Heche, anasema chama hicho bado kina nafasi ya kushiriki kwenye uchaguzi mkuu wa 2025, na kwamba kutosaini kanuni za maadili hakuwaondoi kikatiba kushiriki uchaguzi, kwani hakuna muda wa mwisho wa kusaini — wanaweza kufanya hivyo siku yoyote watakayotaka.

Aidha, Heche amesisitiza kuwa msimamo wa CHADEMA mpaka sasa ni "NO REFORMS NO ELECTION".

Nadhani viongozi wa CHADEMA wangeacha kuongelea habari za uchaguzi maana wameshakataa hawatoshiriki na kanuni hawakusaini.
 
Sitaki nataka kama unatongoza demu wa kijijini
 
Kikatiba mbunge anatakiwa awe mwanachama wa siasa. Wabunge 19 wamefukuzwa na chama chao kwa hiyo kupoteza sifa za kuwa wabunge. Mwezi wa 6 wanamaliza ngwe yao kama wawakilishi wa chama chao wanaotambuliwa na Bunge.
Matamko kama haya ndio yanaonyesha kuwa hamna Plan B. Kwa kusema aliyosema ni kuwa wanaamini kuwa ukarabati wa Katiba na taratibu za uchaguzi utafanyika kabla ya Bunge kuvunjwa. Hawako serious.

Amandla...
Sikilizeni... Muhimu kuliko yote ni kusimamia ukweli!
Hakuna haja ya kushiriki chaguzi zilizojaa utapeli na wizi!
Ukiangalia kwa karibu kwa sasa kila mtu kokote aliko anawaza udanganyifu... Wanafunzi, wafanyakazi, wachungaji, masheikh, wachezaji, n.k. Yote ni matokeo ya mifumo yetu ya siasa na uchaguzi kulea ufisadi, utapeli na wizi!
Yaani kifupi ni bora kupata hata kama ni kwa njia haramu!
 
Back
Top Bottom