Tetesi: John Heche kumrithi Freeman Mbowe Uenyekiti CHADEMA

Tetesi: John Heche kumrithi Freeman Mbowe Uenyekiti CHADEMA

Nani alikuambia CHADEMA ni ya Watanzania? CHADEMA ni mali ya Familia ya Mtei na mkwewe Freeman Mbowe. Nyie wengine ni wasindikizaji tu au kwa kiingereza cheerleaders Mbowe ni Mwenyekiti wa chama toka 2003 wakati wa Mkapa. Na kila aliyethubu kugombea alionja sumu kwa kidole
Pumbavu kabisa
 
Mleta uzi acha upuuzi. Chama cha familia anapewaje mtu baki kama Heche? Hujui kuna James Mbowe na yule binti aliyejitokeza kwenye maandamano juzi? James na dada yake wakishindwa kuna John Mrema. Huyo Heche aendelee kuwa mwanaharakati kama mdude.
Wacha ukahaba
 
John Mrema kaoa toka ukoo wa akina Mbowe aisee
Na wewe umeolewa kwenye ukoo gani huko Uchagani? Maana tangu Mbowe akupige kibuti umeshindwa ku move on unamuwaza yeye tu utafikiri wewe ndiye mwanamke wa kwanza kutolewa usichana halafu mwanaume akuache.
 
Ngoja tuone hii ya Heche kama ni kweli
Ni chama kaanzisha mkwe wake Edwin Mtei, unataka aachie aende wapi? Hii akitoka yeye inakwenda kwa mwanaye Dudley. Hawa wengine wote kina Mnyika, Lissu, Martin, Lema ni cheerleaders tu
 
Siko Mbowe alipoitisha maandamano na kusema SAMIA MUST GO na baadae kujikuta Yuko peke yake na Vijana wa CHADEMA wakaanza kusema MBOWE MUST GO,

Naona Mbowe akiondoka kabla ya Rais Samia
MBOWE MAUST GO
 

View attachment 3122169
Mwenyekiti wa wakati wote na wakudumu wa Chama kikuu Cha Upinzani nchini Tanzania Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Freeman Aikael Mbowe huenda akung'atuka kwenye nafasi hiyo ya uenyekiti wa Chama hicho ngazi ya Taifa aliyoihudumu kwa zaidi ya miongo mitatu mapema mwezi ujao.

Habari za chini chini toka CHADEMA zinasema huenda Freeman Aikael Mbowe atakuwa na imani zaidi endapo tu atakiacha chama hicho chini ya John Heche Mkurya toka Tarime kijanq jasiri wa muda mrefu mwenye misimamo thabiti isiyoyumba wala kutetereka au kutetereshwa hasa katika kusimamia haki na rasilimali za Watanzania bila kujali itikadi zao.

Duru za siasa nchini Tanzania zinasema John Heche ambae pia ni Mbunge mstaafu wa Jimbo la Uchaguzi la Tarime Vijijini ndio kijana pekee kati ya Vijana wote waliorithishwa nafasi ya uenyekiti wa BAVICHA( wing ya vijana) na Freeman Mbowe aliyeweza kuiongoza taasisi hiyo kwa Mafanikio zaidi na kuifanya BAVICHA | CHADEMA kupata imani kubwa toka kwa makundi na watu mbalimbali hasa ya Vijana waishio nje na ndani ya Tanzania.

Taarifa zinaonesha John Heche ndio mwanasiasa pekee wa Upinzani aliyeahidiwa na kutamanishwa mambo mengi zaidi na mazuri ikiwemo nafasi ya Uwaziri na aliyewahi kuwa Rais wa Tanzania awamu ya tano Hayati Dkt John John Joseph Pombe Magufuli huku taarifa zikidokeza kuwa alikataa kata ofa zote hizo zilizoelekezwa kwake ili kuihama na kuisaliti CHADEMA.

Mwanasiasa John Heche anatazamwa na WanaChadema walio wengi nchini Tanzania kama mtu pekee anayeweza kuhamasisha kundi kubwa la watu hasa vijana wasio na ajira na mafukara wa vipato kujiunga na Chama hicho na hatimaye 2025 CHADEMA iweze kushinda na kuongoza Serikali | Dola 2025-2030 kupitia Uchaguzi huru na haki utakaofanyika nchini Tanzania baadae mwakani huku Upinzani mkali ukitarajiwa kati ya Tundu AM Lissu wa CHADEMA na Rais wa Sasa wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan toka chama tawala cha CCM.

Soma Pia: Ni kweli Mbowe hawataki Lissu, Heche, Lema, Msigwa na Wenje ndani ya CHADEMA?

John Heche anayetajwa kuwa swaiba mkubwa wa Ndg Tundu AM Lissu na mwanasiasa asiye na chembe ya woga wa ama kufa ama kuishi duniani anaonekana kuwa mwiba mkali na mchungu kwa Upande wa Chama Cha Mapinduzi CCM kiasi Cha CCM kumtamani Freeman Mbowe aendelee kuwa Mwenyekiti wa Chama hicho kwa muhula mwingine tena wa miaka mitano ( 2024-2029 ) huku Lissu akisalia kuwa Makamu wake na Mgombea wa Urais 2025 kama alivyokwisha kutangaza nia yake hiyo.

Hata hivyo vijana wanaotaka mabadiliko ndani ya CHADEMA hasa wasomi wameendelea kumsihi Freeman Mbowe akae pembeni ili kupisha damu changa na zaidi sana kuionesha Dunia demokrasia wanayoihubiri nje na ndani ya Chama hicho kwa vitendo.

Pamoja na hayo vijana wanufaika wa Bwana Freeman Mbowe kama ilivyokuwa kwa vijana wa Hayati Mwl Julius Nyerere walivyomgomea Mwl Nyerere kung'atuka madarakani kwa kisingizio kuwa nchi ni changa ndivyo hivyo ilivyo leo kwa vijana wa Freeman Mbowe wanamwambia kuwa asithubutu kuachia Chama kwa sasa kwani chama bado ni kichanga sana huku baadhi yao wakiwatazama wao na familia zao kuwa ndio wachanga ila si CHADEMA hasa wakati huu ambapo chama hicho kikiendelea kuzorota siku baada ya siku kiasi Cha wanachama kugoma hata kuandamana jambo ambalo halijawahi kushuhudiwa tangu kuasisiwa kwa Chama hicho nchini Tanzania chini ya mamlaka hizo hizo za Serikali ya Tanzania (Polisi )

Kijana John Heche anatajwa kama kijana mwenye mvuto zaidi ndani na nje ya CHADEMA kwa Sasa na huenda ndio mtu pekee atakayeweza kumwangusha Freeman Mbowe kwenye sanduku la kura mapema mwezi ujao endapo tu Freeman Mbowe atasalia kuwa king'ang'anizi wa kiti hicho kwa miaka mingine mitano ili kutimiza mihula sita inayofanya jumla ya miaka 30 uongozini akivunja rekodi ya Hayati Augustino Lyatonga Mrema aliyefia madarakani.

[CHADEMA tunawatakia kila lenye heri kuelekea uchaguzi wenu huu Mkuu wa Chama na Serikali sisi tusio na chama tunahitaji kuona Upinzani imara ili kujenga Serikali madhubuti ya Tanzania]

View attachment 3121911
Huyu ndie John Heche Mwenyekiti mtarajiwa wa CHADEMA 2024-2029 katika moja ya mikutano yake.

Heche aje CCM tufanye kazi anakipaji kikubwa sana Cha uongozi
 
Back
Top Bottom