John Heche: Kuna mpango wa Watu kupewa pesa ili kuvuruga Mkutano wa Baraza Kuu CHADEMA

John Heche: Kuna mpango wa Watu kupewa pesa ili kuvuruga Mkutano wa Baraza Kuu CHADEMA

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA (Bara), John Heche, ameibuka na kudai kuwepo kwa "mipango miovu" inayoratibiwa na baadhi ya waliokuwa wanachama na viongozi wa zamani wa chama hicho kuelekea Mkutano wa Baraza Kuu la CHADEMA.

Akizungumza leo Agosti 29, 2026, katika Makao Makuu ya Chama, Heche ameeleza kuwa watu hao wanafanya "biashara ya udalali wa siasa" kwa kutoa fedha ili kuvuruga vikao halali vya chama.

Heche amebainisha kuwa lengo kuu la mikakati hiyo ni kuvuruga Baraza Kuu kwa kutumia fedha, lakini akawatoa hofu wanachama na viongozi kwa kueleza kuwa uongozi unafuatilia kila hatua na "fedha hizo zitaishia kuliwa tu" bila kufanikisha azma hiyo. Amesisitiza kuwa CHADEMA inalindwa na wananchi na ndio tumaini pekee lililobaki kwa nchi.

 
HQaE0G2WYAAue2n.jpg
 
Back
Top Bottom