John Heche: Kuna vitisho vikubwa sana kuhusu uhai wangu, Serikali ichukue Tahadhari

John Heche: Kuna vitisho vikubwa sana kuhusu uhai wangu, Serikali ichukue Tahadhari

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Tanzania Bara, John Heche, amesema amekuwa akikabiliwa na vitisho vinavyolenga usalama na uhai wake kutokana na shughuli zake za kisiasa. Heche amesema vitisho hivyo ni vya kiwango kikubwa kiasi cha kumfanya kuiomba Serikali kuchukua tahadhari ili kuzuia madhara yanayoweza kujitokeza.

Akizungumzia hali hiyo, Heche amesema, “Kumekuwa na presha kubwa sana ya vitisho. Tisho kuhusu uhai wangu,” huku akieleza kuwa baadhi ya vitisho anavyopokea hawezi kuvipuuza. Amesema kazi anazofanya ni za kisiasa na za utetezi wa wananchi, hivyo hazipaswi kuwa sababu ya mtu kutishiwa maisha.

Daah hivi hawa viongozi wataendelea kulalama hivihadi lini?
Yaani unalalamika na unataka serikali ichukue tahadhari wakati wanaokuja kuteka watu wanakuja wakiwa na magari, silaha za moto na pingu za serikali!
Daah! Very Illogical!
 
Serikali ndio mtuhumiwa kwahiyo asitarajie watachukua hatua yoyote.
Aishi kwa kujilinda sio kwa kuwaza hii serikali itamlinda na uzuri hata mwenyewe anajua nani ni adui yake.
Serikali ni kikundi cha watu chenye wajibu wa kuongoza nchi au taifa.
Huo wajibu ni pamoja na;
1. Kuhakikisha usalama wa wananchi na mali zao kwa mujibu wa sheria.
2. Ulinzi dhidi ya maadui wa nje (mipaka, wizi wa raslimali, uvamizi na aina zote za ukoloni, hasa Mambo Leo kwa nyakati hizi).
3. Kuhakikisha huduma za jamii kama making, elimu, afya, miundombinu inapatikana kwa wananchi.
4. Kusimamia uchumi (Kodi, maliasili zote n. k.

Kwa nchi yetu, kwa mujibu wa katiba, madaraka yote yapo kwa wananchi, hivyo serikali inapaswa iogope wananchi na siyo kinyume chake.
Wananchi wamepewa uwezo kikatiba kuishughulikia serikali kama inaenda kinyume na mahitaji yao.
 
Back
Top Bottom