Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, John Heche, amesisitiza kupitia mitandao ya kijamii kwamba maendeleo hayawezi kuwa kisingizio cha kutofuata sheria, kuharibu demokrasia au kuendeleza uchawa.
Kupitia chapisho la leo Machi 18, 2026, Heche amesema kuwa vitendo vya kuharibu bunge la Wananchi au kutozingatia sheria havikubaliki, bila kujali kiwango cha maendeleo kinachodaiwa kufanikishwa.
“Maendeleo hayawezi kuwa kisingizio cha kutofuata sheria, kuua demokrasia, kuleta uchawa, kuua Bunge la Wananchi nk,” amesema Heche. Ametoa wito kwamba maendeleo ya kweli yanapaswa kuwa kwaajili ya binadamu, si binadamu kwaajili ya maendeleo.
“Hakuna maendeleo yanayoweza kulinganishwa na uhai wa mtu. Maendeleo ni kwaajili ya binadamu, sio binadamu kwaajili ya maendeleo… watu wote wakifa hakutakua na maji, wala umeme wala barabara,” amesisitiza John Heche.
Aidha, Heche ameeleza wazi kuwa inawezekana kwa kiongozi kuwa bora, akifuata sheria, kujenga demokrasia na kuleta maendeleo makubwa bila kuingilia misingi ya haki na demokrasia