John Heche: Magufuli alikuwa bora kusimamia rasilimali na kurekebisha ujinga

Ni kweli, hata siasa za kutekana na kupora uchaguzi mzima JPM ndio muasisi. Kama ni maendeleo hata kagame, Idd Amin, Gadaffi walifanya maendeleo makubwa ya kiuchumi ila kilichowaharibia ni utawala wa kidilteka na mauaji.
Kabisa, hawa wajinga hawajui kuwa tunajua tumefikaje hapa. Huu uhuni kwenye demokrasia yetu ni ushenzi uliopandwa na Magufuli. Kama kuna kuna sehemu alizopatia huo ulikuwa wajibu wake na wala sio hisani. Ila uovu alioupanda kwenye nchi hii haikuwa sehemu ya majukumu yake, bali ni ukatili na ulevi wa madaraka. Hii kauli ya Heche wanataka kufanya ni kama kamsifia Magufuli, na wala sio kuweka record sawa.
 
"mtanikumbuka" alisikika akisema.
 
nafikiri chadema waache kuzungumza Mambo ya magufuli
Kabisa, maana kauli zao zinaweza kutumika kupotosha wenye akili ndogo. Sioni kama watu wengi wanauelewa wa record zikiwekwa sawa. Maana kama watu wanaletewa miradi ya maendelea kwa fedha za umma, kisha wanaambiwa ni fedha za rais na wanaamini ni hisani yake, watu kama hao hawa wakiwekewa record sawa ni kuwachanganya tu.
 
Mwambie heche
 
JPM alipatia mengi kuliko makosa.
 
Hiyo mikataba ya rasilimali si mlimpiga vita alipokuwa akizuia kwa kusema mtashtakiwa? Hakuna hata jema moja mlilopongeza kwake. Kukiri kipindi hichi ni unafiki wa kiwango cha SGR rail ya kuunganisha mabara
Mtazamo wa Lisu na wa Heche ni tofauti kwenye eneo hilo.
 
Wananchi ndo wenye maamuzi ya kuitoa CCM. Mpaka leo unawategemea wanasiasa kuja kukuletea ukombozi,,hawa ambao wanahama hama vyama.

Ni maamuzi ya wananchi siyo vyama,
Halafu kuhama chama sio kosa la jinai , hiyo ni best na common practice ambayo ipo dunia nzima.
 
Hiyo mikataba ya rasilimali si mlimpiga vita alipokuwa akizuia kwa kusema mtashtakiwa? Hakuna hata jema moja mlilopongeza kwake. Kukiri kipindi hichi ni unafiki wa kiwango cha SGR rail ya kuunganisha mabara
Magufuli lini aliwahi kuwasifia cdm, kuna sera ya elimu Bure ccm waliiga kutoka kwa cdm, ni lini Magufuli aliwahi kukiri kuwa hilo lilikuwa jambo jema na wameiga cdm?
 
Zamani walisema haya ,pumbavu zao

USSR
 
Hata Magufuli alipopora uchaguzi wa 2020 watu wangeandama angewaua. Ni bahati tu watu hawakuwa na ujasiri kama wa juzi. Ni mara ngapi Magufuli alikuwa anatishia watu na kujaza jeshi ili liwaumize wananchi waliotaka kuandamana? Hatujasahau.
Magu alikuwa muwazi na mkweli kwamba atawafyeka miguu.
Mrithi wake akasema hakutakuwa na nywi nywi wala nywinywinywi.
 
JPM alipatia mengi kuliko makosa.
Upo sahihi kwa mtazamo wako ila sasa ungekua mtoto wa Lissu na kuona baba yako anamiminiwa riasi 36 ungekuwa na mtazamo chanya? Chadema walipigika sana so tuwaelewe tu kuwa upande mbaya wa JPM ndio wanauona zaidi pengine kuliko raia kama wewe ambaye hujawahi kukutana na mkono wa JPM moja kwa moja.
 
Magufuli lini aliwahi kuwasifia cdm, kuna sera ya elimu Bure ccm waliiga kutoka kwa cdm, ni lini Magufuli aliwahi kukiri kuwa hilo lilikuwa jambo jema na wameiga cdm?

Magufuli lini aliwahi kuwasifia cdm, kuna sera ya elimu Bure ccm waliiga kutoka kwa cdm, ni lini Magufuli aliwahi kukiri kuwa hilo lilikuwa jambo jema na wameiga cdm?
Kwani hapa tunalinganisha kusifia upande fulani na fulani au tunajadili kumsifia mtu akiwa kafariki na kumsema vibaya akiwa hai.

Hebu acha mhemko ya kulazimisha kutafuta kosa kuonekane sawa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…