John Heche: Magufuli alikuwa bora kusimamia rasilimali na kurekebisha ujinga

John Heche: Magufuli alikuwa bora kusimamia rasilimali na kurekebisha ujinga

Acheni kauli za jumla, mbona walimsifia alipokamata kina Seth wa IPTL, alipotenganisha wizara ya madini na nishati, alipozuia wezi wa Tanzanite, pia alipokataa mkataba wa bandari ya bagamoyo. Mbona mara kibao tu walimpongeza ila ukosoaji wa chadema ulikua kwenye kuminya demokrasia ambayo iliwaathiri chadema moja kwa moja.

Acheni kauli za jumla jumla mkienda kwenye specifics utajua wapi JPM alipatia wapi alikosea.
Tatizo la wafuasi wa magufuli hawakubalk kuwa alikuwa na makosa. Wao hupenda aongelewe kwa mazuri tu as if alikuwa malaika🙆‍♂️
 
Kwani hapa tunalinganisha kusifia upande fulani na fulani au tunajadili kumsifia mtu akiwa kafariki na kumsema vibaya akiwa hai.

Hebu acha mhemko ya kulazimisha kutafuta kosa kuonekane sawa.
Issue hapa ni kusifia boss, na si ajabu angasemwa vibaya ungesema marehemu hasemwi vibaya. Alipokuwa hai alipewa ukweli wake. Na kwa kukusaidia tu, Heche hajamsifia Magufuli bali ameweka record sawa.
 
Kabisa, hawa wajinga hawajui kuwa tunajua tumefikaje hapa. Huu uhuni kwenye demokrasia yetu ni ushenzi uliopandwa na Magufuli. Kama kuna kuna sehemu alizopatia huo ulikuwa wajibu wake na wala sio hisani. Ila uovu alioupanda kwenye nchi hii haikuwa sehemu ya majukumu yake, bali ni ukatili na ulevi wa madaraka. Hii kauli ya Heche wanataka kufanya ni kama kamsifia Magufuli, na wala sio kuweka record sawa.
Kwani mkuu mtu akitimiza wajibu wake si anastahili kusifiwa kwa sababu wengi hawawezi kutimiza huo wajibu
Ndio sababu kwa nini wanafunzi wakifaulu wanasifiwa hata kama ni wajibu wao kufanya vizuri kwenye mitihani. Sio sahihi kusema Magufuli hastahili sifa eti kwa kuwa ni wajibu wake
 
JPM alipatia mengi kuliko makosa.
Sahihi JPM alikuwa Rais bora sana, sure alikuwa anakandamiza vyama pinzani tena sio too much kama anavyofanya Samia, ila Magufuli alikuwa anaipenda nchi yake, alijua kukomesha mafisadi, alijua kusimamia miradi, alijua kujenga nchi yani alikuwa anaelewa Tanzania inastahili nini
Sio kama Samia anaboronga kila kitu. Mpaka sasa hata sijui Manyonyo yuko vizuri kwenye nini
 
Yaani hata nyuzi za kutumia akili mabumunda ndiyo huanza kuzidaka na kuzitapikia kabla watu timamu hawajaingia kufafanua. Na bahati mbaya hata yakifafanuliwa huwa hayaelewi!

Alichokizungumza Heche wala hakihitaji akili ya kindergarten kukielewa, ila mijinga iliyomwona jiwe kama bwana yao imeuwahi uzi huu na kulitia aibu taifa (mijitu yenye akili kisoda ni aibu ya taifa) bila hofu yoyote. Na hata watu wenye akili walipokuja kufafanua sana bado hayaelewi chochote! Pumbafff.
 
Kama asingeminya upinzani trust me hata chadema isingesimamisha mgombea 2020 na mpaka leo angekua hai. Tatizo yeye badala ya kupambana na mafisadi yaliyojaa CCM akapambana na upinzani ambao haujawahi kula hela ya hazina.
Jpm alikuwa bize na kuua jongoo yaani aliamini chadema ni maadui binafsi nilimdharau sana yaani unahangaika na wabunge na madiwani wa chadema kama maadui ilihali kulikuwa na nyoka kibao wamejaa huko ccm
Matokeo yake nyoka wakamngata ila minawalaumu sana wakina polepole, bashiru hawa ni watu wake wa karibu kwànini hawakumwambia ukweli kwamba adui zake wapo ndani

Alafu baada ya kufa polepole anakuja kutulilia mitandaoni ilihali huna mamlaka alishindwa nini kumshauri jpm
 
Kwani mkuu mtu akitimiza wajibu wake si anastahili kusifiwa kwa sababu wengi hawawezi kutimiza huo wajibu
Ndio sababu kwa nini wanafunzi wakifaulu wanasifiwa hata kama ni wajibu wao kufanya vizuri kwenye mitihani. Sio sahihi kusema Magufuli hastahili sifa eti kwa kuwa ni wajibu wake
Mshahara ndio muhimu, sifa ni hisani isiyodaiwa.
 
Upo sahihi kwa mtazamo wako ila sasa ungekua mtoto wa Lissu na kuona baba yako anamiminiwa riasi 36 ungekuwa na mtazamo chanya? Chadema walipigika sana so tuwaelewe tu kuwa upande mbaya wa JPM ndio wanauona zaidi pengine kuliko raia kama wewe ambaye hujawahi kukutana na mkono wa JPM moja kwa moja.
Kwahy unataka niongee kama nani, kama mtoto wa lissu au mwananchi?
 
Nyie endeleeni kumkosoa kulingana na makosa yake, ila mm nimeamua kumsifia kutokana na mazuri.
Usinipangie.
Nani kukuzuia kumsifia, hiyo ni haki yako hakuna mwenye tatizo na hilo. Ila kudhani kuwa Heche ni mjinga kwamba kuweka record sawa ni kama anamsifia Magufuli, basi ujue kiwango chako cha uelewa ni kidogo.
 
Heche alisema kuwa katika upande wa kusimamia baadhi ya mambo ya rasilimali na kujaribu kurekebisha kile alichokiita "ujinga wa mikataba" uliokuwepo huko nyuma, Magufuli alionyesha nia na kujitahidi, akisisitiza kuwa jambo hilo ni lazima lisemwe kwa uwazi bila kuficha ukweli.
Hivi ni yeye alisema "Mtanikumbuka"?

Katika haya yaliyosemwa na Heche; na tukiyaunganisha na yanayofanywa na Samia Suluhu Hassan hata mimi "NAMKUMBUKA John Pombe Magufuli"; hata bila kusahau yaliyomchafua vibaya sana kama kiongozi wa nchi.
 
Kwahy unataka niongee kama nani, kama mtoto wa lissu au mwananchi?
Ndio nasema kwa mtazamo wako JPM yuko vizuri maana uliona mema yake ila wanachama wa chadema tuliona makali yake so tunaona upande wake mbaya. So kila mtu abaki na maoni yake ndio maana hata Mandela licha ya kupigania uhuru na kupendwa sana Afrika kusini ila takribani 40% ya wapiga kura walimkataa kwenye uchaguzi wa Urais.
 
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, John Heche, ametoa uchambuzi wake kuhusu jinsi viongozi waliopita walivyoshughulikia rasilimali za nchi.

Heche akiwa Kilwa mkoani Lindi, Juni 3, 2026 alikiri kuwa ingawa walikuwa na tofauti kubwa ya kimtazamo kuhusu masuala ya demokrasia na haki za kisiasa, kuna maeneo ambayo Magufuli alijitahidi kufanya vizuri.

Heche alisema kuwa katika upande wa kusimamia baadhi ya mambo ya rasilimali na kujaribu kurekebisha kile alichokiita "ujinga wa mikataba" uliokuwepo huko nyuma, Magufuli alionyesha nia na kujitahidi, akisisitiza kuwa jambo hilo ni lazima lisemwe kwa uwazi bila kuficha ukweli.

Hapo Heche nakuunga mkono! Madhaifu ya JPM ni machache ukilinganisha na mazuri yake
 
Back
Top Bottom