John Heche ni kiongozi makini sana

John Heche ni kiongozi makini sana

Kinumbo

JF-Expert Member
Joined
Dec 8, 2019
Posts
3,039
Reaction score
5,560
Mimi sio mwanasiasa ila kuna kitu nimeona kwa huyu mwamba.

John Heche kwa sasa ni Makamu mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA). Huyu mzee ameonyesha umahiri mkubwa sana toka akiwa mbunge mpaka sasa kuwa makamu mwenyekiti, nimekuwa nikimfuatilia na kujidhihirisha vya kutosha kuwa ni makini sana.

Heche amekuwa mzungumzaji mzuri pale anapo pewa wasaa wa kuzungumza, mkweli na mwenye kujenga hoja kikamilifu. Hotuba zake zimekuwa za kuvutia na zenye mashiko, Heche ni mzalendo na mpenda maendeleo kwa nchi yake. Amekuwa akiikosoa serikali wazi wazi bila kuhofia chochote kile, huyu mwamba anafaa kuwa zaidi ya hapo.

Chadema hakika wamepata mtu sahihi na makini, nawashauri baada ya hiyo kampeni yao inayo endelea endapo ikazaa matunda mazuri basi mgombea wa urais wamsimamishe Heche. Heche anafaa kuwa rais wa nchi hii maana ana sifa zote. Hotuba ama interview za huyu mwamba ukisikiliza hutamani ata ziishe, yule mkurya ni kichwa haswa.


View: https://m.youtube.com/watch?v=wbDBGPMllm4&t=535s [HECHE ASIMULIA ALIVYOKOSA POSHO ya MIL1 kwa SIKU - BUNGE la NDUGAI TIMUATIMUA ya WABUNGE wa UPINZANI - YouTube] The hottest video right now, don't miss it. (Sharing from UC Mini)
 
Back
Top Bottom