Naunga mkono hoja yupo zaidi kitaifa. Hoja zake ni za msingi, za Kimagufuli.Nimefuatilia sana mikutano ya Ndugu John Heche ( Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA taifa) haya ndiyo niliyoyabaini:-
1. Ndiye mwanasiasa pekee bora kwa sasa mwenye ushawishi wa hoja zote anazosimamia.
2. Ni mwanasiasa mwenye uwezo mkubwa wa kuelewesha wananchi ambao wengi uelewa ni mdogo na wakaelewa. HECHE ameibua nguvu kubwa ya uungwaji mkono toka kwa wananchi.
3. Ni mtu anayejikita kwenye hoja za pamoja kuliko shida zake bonafsi.
4. Anajiamini kwa kile anachokisimamia.
Hoja zote za CHADEMA zina kusudi jema na Taifa letu🇹🇿.
Tusimame na CHADEMA.
#NoReformsNoElection#
Chawa hukaa pachafu. We mchafu na hujatahiriwa kisiasa. 🚮John Heche ni mwanasiasa wa hovyo. Wanasiasa makini hawashambulii kundi muhimu la wapiga kura ambao ni wanawake. Heche aliamuru baunsa wake ampige katibu mwenezi mwanamke. Majuzi hapa kamshambulia mwanamama Suzan Kiwanga kwa kauli za hovyo mno. Heche anakiharibia zaidi CHADEMA badala ya kukisaidia.
Dua la kukuChawa hukaa pachafu. We mchafu na hujatahiriwa kisiasa. 🚮
Ipo siku mtalipa haya myafanyayo kwa kujitoa ufahamu.
Hakika mkuuHeche anagusa mambo yanayomhusu mwananchi moja kwa moja ndiyo maana anaeleweka vizuri sana.
Siku Lissu akijiadjust akaweza kubalance hoja za kisheria, haki, utawala bora (vitu ambavyo anavimudu sana) NA mambo ya uchumi kama vile kilimo, biashara, ajira za watu, rasilimali za nchi na matarajio ya vijana Ushawishi wake utakuwa maradufu.