John Heche: Sheria ndizo zinaruhusu mikutano ya kisiasa na si polisi

John Heche: Sheria ndizo zinaruhusu mikutano ya kisiasa na si polisi

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Ikiwa imepita siku moja tangu Jeshi la Polisi lifungue milango ya kupokea taarifa za nia ya kufanya mikutano ya hadhara kutoka kwa vyama vya siasa na wadau wengine kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu zilizopo kutokanana hali ya usalama kuelezwa kuendelea kuwa shwari,Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, John Heche amewataka viongozi wa chama hicho mkoa wa Simiyu kuandaa mkutano mkubwa wa hadhara ndani ya siku chache zijazo.

Akizungumza leo kwenye Mkutano Mkuu Maalumu wa CHADEMA Mkoa wa Simiyu uliofanyika Bariadi Mjini, Heche amedai kuwa kurejeshwa kwa ruhusa ya kufanya mikutano hiyo siyo kwasababu ya matakwa ya Jeshi la Polisi bali ni kwa mujibu wa sheria na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Soma Pia: DCP Misime: Hali ya Usalama nchini ni Shwari, wenye nia ya kufanya mikutano wawasilishe taarifa kwa wakuu wa polisi wa wilaya

Kauli ya Heche na Jeshi la Polisi zinakuja mwezi mmoja tangu serikali kupitia Waziri wa Mambo ya Ndani, Patrobas Katambi kutangaza kusitisha kwa muda mikutano yote ya hadhara ya vyama vya siasa nchini, bila kujali chama husika, ikieleza kuwa hatua hiyo inalenga kuimarisha usalama wa wananchi.

 
Back
Top Bottom