Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Heche, akiwa mkoani Morogoro katika ziara ya oparesheni, amesema: "Bila mabadiliko hakuna Uchaguzi, ndiyo oparesheni ya Chama chetu."
Ameeleza kuwa: "Nchi hii imejaa propaganda, nchi imejaa uongo, vyombo vya habari vinasambaza uongo. Magazeti, TV, redio na uongo usipojibiwa, ukiachwa sana watu wanaweza kuuamini. Ukifunguliwa redio nchi hii, ukisikiliza mambo yanayosemwa kwamba ameyafanya Rais Samia unaweza ukafikiri nchi hii ni Marekani au Uingereza."
Ameongeza: "Kwingine nimepita wameandika mabango wanasema 'Mama hatukudai', hapa kwenu hayapo? Hakuna sehemu wamebandika hayo mabango? Mama hadaiwi! Nani kama Mama, siku hizi mtu akikohoa hata kikohozi utasikia 'Kikohozi cha Mama!' Mvua inanyesha tunamshukuru Mama ametuletea mvua! Nyie hamjamsikia huko? Na hewa tunayoivuta hii, hivi karibuni tutaambiwa hewa ya Mama na Milima ya Udzungwa ya Mama, milima ambayo ipo miaka yote saa hizi ya Mama Samia."