Pre GE2025 John Heche: Tumeamua kuhakikisha kwamba uchaguzi haufanyiki. Tutawashirikisha Viongozi wa dini, mashirika ya kimataifa, balozi na NGO's

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Wajiandae na uchaguzi ili iweje?
 
Hiyo ni agenda ya mfukoni ya mwenyekiti. Na ndio maana wanachadema hawaielewi wapo wanatoa macho
 
Unataka Chadema ishiriki uchaguzi mbovu ili iweje?
 
kwa hiyo kama uchaguzi hautafanyika, hasara kwa nani sasa? manake Samia ataendelea kuwa Rais wao kwa miaka mingine kadhaa bila kuchaguliwa hadi uchaguzi uje ufanyike. Samia hapo anatikisa tu mkia wala haathiriki na chochote, ndio kwanza mmemsaidia aendelee kuwatawala.

ninachowashauri, tufanye tu uchaguzi kwa sababu kitu pekee chadema watakipata sio urais, ila wabunge wengi sana watakaokuwa na influence na pia watakuwa na ruzuku ya kutosha. wapiganie ruzuku tu hapo sio kuchukua nchi. sasa wakisema hawafanyi kabisa uchaguzi nataka kuamini wamepewa sukari ili kumsaidia maza aendelee kuwepo madarakani bila kuchaguliwa.
 
Wanaoshiriki uchaguzi ni wao, wanaokabiliana na dhuruma za uchaguzi ni wao, wanaojua hata uchaguzi ukifanyika leo kwa sheria za uchaguzi zilizopo watadhurumiwa ni wao.
Unayewaona wapumbavu! Nadhani wewe ndiye mpumbavu kuliko wao.
Waache wapinganie wanachoamini na uzuri wanaosimamia sheria hizo wanasema ni kweli lakini muda hautoshi.
Kama ungekuwa siyo mpumbavu ungewashauri hao unaowaona siyo wapumbavu wawasikilize malalamiko yao
 
Kujiandaa na uchaguzi wa wizi?Hakuna uchaguzi mpaka wezi wote wamulikwe na kuondolewa
 
Gentleman,
utapeli wa kisiasa ukifanywa na vibaka wa kisiasa hua unafanyika kihivyo sana,

kwahivyo viongozi wa dini, mabalozi, NGO's na mashirika ya kimataifa ndiyo yanapiga kura?

kwamba hao ndio wanaweza kuvunja katiba pasiwepo na uchaguzi?🤣

ndezi sana dah 🐒
 
Shida ya Chadema ni kama wanadhani chama ni wao tu hawajui CCM wanawaza mbele yao, wanaweza kugomea haki yao ila hawawezi kuzuia na wajue kuna vyama vingi vya kwenye mabegi watashiriki na machoni wataonekana wameshiriki. Kununa wala sio issue ila kuzuia uchaguzi wataishia sehemu mbaya tu sheria zipo na wala hakuna atakayekuja kuwaokoa. Nadhani wangetafuta viti vingi bungeni ila walete upinzani mkubwa kisheria, shida yao wanaota wachukue nchi kirahisi hivi, bado mfumo unaibeba sana CCM huwezi kupindua meza tu kama uko Bar.
 
Kwahyo unataka waingie ktk uchaguzi ili waibiwe kula kama ilivyokuwa ktk uchaguzi uliopita sio"ujinga ni wakati wa kwenda tu"
 
MBowe alisema hivi hivi

Akaonjeshwa. Pesa za billicanas akagusa kale kanakopokelewa kila mwezi aka ruxuku

Huyoooo yumoo SERKL za mitaa mkaishia kuaibika kila konaaaa

Sijui wewe unawahahakikishiaje watanzania hutobadili haya maneno kama MJOMBA aikael
 
Hela ya kuendesha shughuli za kila siku za chama hawana, sasa wanatembeza bakuli hawawezi kushiriki uçhaguzi acha wakae pembeni wawaache wenye uwezo.
 
Kwahyo unataka waingie ktk uchaguzi ili waibiwe kula kama ilivyokuwa ktk uchaguzi uliopita sio"ujinga ni wakati wa kwenda tu"
Kwenye uçhaguzi hakuna kula. Njaa zenu mnawaza kula tuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…