SI KWELI John Heche tupo kwenye hatua nzuri ya mazungumzo na serikali

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Kumekuwepo na chapisho linalosambazwa kwenye mtandao wa Facebook likiwa na nukuu inayodaiwa kumhusu Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA taifa John Heche Katika chapisho hilo, Heche anadaiwa kusema kuwa wako katika hatua nzuri ya mazungumzo na serikali.

Aidha, chapisho hilo limesambazwa kupitia vikundi mbalimbali vya Facebook, likidaiwa kuwa limetolewa na ukurasa wa Jambo TV. Ujumbe uliobebwa katika chapisho hilo unasema:

“Tupo kwenye hatua nzuri ya mazungumzo na Serikali kuelekea maridhiano ya kitaifa yenye lengo la kuimarisha mshikamano, kulinda maslahi ya taifa, na kuharakisha maendeleo kwa Watanzania wote.” — John Heche, Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA.
Heche   Machi 31.jpg
 
Tunachokijua

Uhalisia wa madai hayo ni upi?

Ufuatiliaji umebaini kuwa taarifa hiyo si ya kweli. Chapisho hilo linaeleza kuwa kauli hiyo ilitolewa tarehe 29 Machi 2026 wakati wa maadhimisho ya kumbukizi ya vurugu zilizotokea katika uchaguzi wa tarehe 29 Oktoba 2025, akisisitiza umuhimu wa mazungumzo ya kitaifa kama njia ya kujenga umoja na mustakabali bora wa nchi.

Hata hivyo, baada ya kufuatilia kwa kutumia maneno muhimu kwenye kurasa rasmi za Instagram na Facebook za Jambo TV, hakuna ushahidi wowote unaoonesha kuwa chombo hicho cha habari kimewahi kuchapisha taarifa hiyo. Hivyo, dai kwamba chapisho hilo limetolewa na Jambo TV si la kweli.

Vilevile, uchunguzi zaidi umebaini kuwa “graphic” iliyotumika katika chapisho hilo haiendani na mtindo wa kawaida unaotumiwa na Jambo TV katika machapisho yake ya mitandao ya kijamii.
Back
Top Bottom