Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
" Miaka kumi na mbili iliyopita Lindi hii na Mtwara waliambiwa mnaletewa utajiri wa gesi, Miaka kumi na mbili iliyopita walichukuliwa Masheikh hapa, Viongozi wa dini na Maaskofu, wakati ule mimi nilikuwa sijaenda Bungeni.
Wakapelekwa Norway, wakapelekwa Malaysia, wakapelekwa na nchi nyingine ambazo watu wake wameendelea kwa mambo ya gesi, wakati ule serikali ikiwa chini ya Rais Kikwete walikopa mpaka Exim Bank ya China zaidi ya Bilioni tisa za Kimarekani ili kujenga bomba la gesi kutoka hapa kwenda Dar Es salaam kwaajili ya kupeleka gesi Dar Es salaam na maeneo mengine, tulikuwa hata hatujaanza mpango wa Bwawa la Mwalimu Nyerere, tukaambiwa gesi ndio mwarobaini wa matatizo ya umeme nchi hii.
Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Umaskini wa nchi hii ni wa kutengenezewa na viongozi tulionao, wamekaa madarakani kwa zaidi ya miaka 63 na Lindi imeuwawa kiuchumi"- John Heche,Makamu Mwenyekiti CHADEMA (bara), Wakati akizungumza na wananchi wa Lindi kwenye Operesheni ya No reforma, no election leo April 04, 2025