Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Shinyanga, Jeremiah John Jilili amechukua fomu ya kuwania ubunge Jimbo la Solwa katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu 2025.
Jilili sasa ni rasmi atamvaa mbunge wa jimbo hilo aliyehudumu kwa miaka 20 sasa Ahmed Salum Ally, na hii itakua ni mara ya pili kwa wawili hawa kuingia katika kinyang'anyiro cha ubunge kwani hata mwaka 2020 kulikua na ushindani mkali baina yao.
Jilili ni mwanasiasa kijana ambaye amekuwa akipata nguvu ndani ya jimbo hilo na Mwaka 2022 alichaguliwa kuwa Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Shinyanga, na pia Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya chama hicho Mkoa wa Shinyanga.