Chakaza
JF-Expert Member
- Mar 10, 2007
- 40,455
- 73,145
Huyu bwana hakika kama wajumbe wa mkutano mkuu wa TFF watamchagua kuwa mjumbe wa kamati ya Utendaji watakuwa wameitendea haki soka ya nchi hii.
John Kadutu maarufu kama "Mgosi" ni mbunge wa Ulyankulu huko Tabora lakini pia amewahi kushika nafasi nyingi za kimichezo kuanzia enzi za vilabu vya RTC katika mikoa mbali mbali na mwisho alikuwa Mwakilishi wa vilabu mkoa wa Mwanza kabla hajashika nafasi aliyo nayo ya Mwenyekiti wa Chama cha soka mkoa wa Tabora.
Kadutu aka Mgosi, ni mpambanaji na asiye kuwa na ukigeugeu katika maamuzi na figisufigisu za soka anazijua na anaweza kupambana nazo. Na katika viongozi wa juu wanaogomea sioni hata mmoja wa kuweza kuiburuza kamati ya Utendaji iwapo Kadutu atakuwepo kama mjumbe.
Tunahitaji mabadiliko ya soka katika uendeshaji wake kwani tumechoka kuburuzwa na kufanya kama TFF kama sehemu ya kutajirikia na kutokuza soka.
Wajumbe John Kadutu huyoooo, kama mnaipenda soka yetu basi mnajua mnapaswa kufanya nini. Navyo mjua Kadutu hatajiingiza kwenye rushwa, na kama kuna mjumbe anategemea kupokea rushwa kutoka kwake ili amchague basi atakuwa amekosea sana.