John Krasinski ndiye 'mwanaume mwenye mvuto zaidi aliye hai' kwa mwaka 2024

John Krasinski ndiye 'mwanaume mwenye mvuto zaidi aliye hai' kwa mwaka 2024

Kafikisha hata wanawake 100 huyo?, kuna mwamba amekuwa sexiest ametembea na wake wa vigogo walikuwa wanampenda wenyewe 400, na imekuwa heri taarifa imevuja, alikuwa anaenda kumpiku Suleiman, mshambuliaji wa wakat wote tangu kuumbwa kwa dunia mpaka sasa
 
John Krasinski ametajwa na jarida la People kama "Mwanaume Mwenye Mvuto Zaidi Aliye Hai" (Sexiest Man Alive) kwa mwaka 2024.

Kwa mujibu wa jarida la "People Magazine" kutoka Marekani, Novemba 11 kupitia onyesho maarufu la "The Late Show" lililoongozwa na Stephen Colbert, Krasinski, muigizaji na mkurugenzi wa filamu mwenye umri wa miaka 45, alitangazwa na kupokea cheo hicho cha heshima.
Chapisho hilo limezua gumzo kwenye mitandao ya kijamii kwani Mpenzi wa Selena Gomez Benny Blanco ali-share video akizungumzia mambo hayo kabla na kufanya wengi kuamini atapewa Cheo hicho cha heshima kinachotamaniwa na wengi.

Mke wa Krasinski, Emily Blunt, ambaye pia ni muigizaji, amefurahishwa na taarifa hiyo na kusema atakapopata nakala za picha za mume wake kwenye jarida hilo, atazibandika nyumbani kwao mjini Brooklyn, ambapo wanaishi na watoto wao wawili, Hazel na Violet.
Kupata cheo hicho kumechangiwa pia na uhusika wa Krasinski kwenye filamu maarufu "The Office," na uongozi wake katika filamu aliyoiandika na kuiongoza "A Quiet Place," pamoja na "Some Good News" ambayo ilifanya vizuri, huku mwaka huu akitoa comedy inayoitwa "IF."
Mwanaume wa kwanza kupokea cheo hiki cha "Mwanaume mwenye mvuto zaidi" alikuwa Mel Gibson, na wengine waliofuatia ni George Clooney, Idris Elba, John Legend, David Beckham, Dwayne Johnson, na Patrick Dempsey wa mwaka jana.
AAAh wapi
Kipimo cha mwanaume ni mwanamke
REF.Baltazarito Engungansky
 
Huyu jamaa alijuta kwenye ile movie ya 13 hours secret soldier of bengaz

Ilikua Libya sio poa
 
Kwenye the covenant jamaa kacheza sana na mwamba "Ahmed"
Ndo mwenyewe lakini? Leo nipo nipo tu nikaona ngoja ni-Google hiyo The Convenant. Ingawaje nimeiiona ya 2023 na Ahmed yupo lakini huyo mwamba wa Tom Clancy's Jack Ryan sijamuona! Au mimi ndo nimemfananisha?!
 
Ila umenisaidia kuifahamu hiyo The Covenant manake nilikuwa siifahamu na ninaishusha hivi sasa
Ni movie na nusu
Hakikisha ni ya 2023 maana IPO na ya 2006
Humo ndani Kuna Jake na Dar Slim
 
Kwenye Covenant sio yeye , huyu jamaa kacheza Jack ryan na 13 soldiers in Benghazi
Uko sahihi na ndio maana alinichanganya maana zote nimeangalia ila kwa sehem wamefanana na Jake wa covenant
 
Back
Top Bottom