John Mashaka Ni Mbunge Mtarajiwa!

Status
Not open for further replies.
I probably need to go some pages back to understand what on earth is going on.. huo muda ndio tatizo..
 

Asante Painkiller.

Lakini, kama kufungia IP address sio dawa kwa sababu mwanachama anaweza kuizunguka IP address hiyo, basi hata kufungia User name nayo siyo dawa.

We nambie, tofauti ni nini kati ya kufungia IP address na User name ? Hakuna. Zote zinaweza kuzungukwa. Lakini ni vigumu zaidi kuzunguka IP address kuliko User name. After all, half of these clowns who resort to the kind of bawdy violations that undermine the forums are so full of turkey stuffing in their heads they couldn't figure how to spoof an IP if you tutored them.

Kingine, unasema hao members watakuwa punished, no, you are not punishing any members, you are punishing the User name! Watu wamejiandikisha leo leo halafu ghafla ghafla wanaanza na matusi kweli wanaweza kuwa wapya hao kweli ? Unajua kabisa sio wapya. Wangekuwa wanafungiwa IP address zao wangefikiria mara mbili. Kama kuna nia ya kupambana na hili janga - sio "nuisance" kama ulivyo characterize hili tatizo - janga linalohatarisha JF basi mnaweza kuchukua hatua madhubuti.

Unless JF ni mradi wa matangazo ya biashara ambayo yanaleta mapato kutokana na idadi ya User names.

Kufungia IP address sio muarobaini lakini ni mtangawizi. Na ukiongeza uwezekano wa kufungia MAC address unazidi kukaribia muarobaini.

Usiku mwema.
 
Orwell's rule for written english:

1.Never use a metaphor,simile,or other figure of speech which you are used to seeing in print.

2.Never use a long word where a short one will do.

3.If it is possible to cut a word out,always cut out.

4.Never use the passive where u can use the active.

5.Never use a foreign phrase, a scientific word,or a jargon word if u can think of an everyday English equivalent.

6.Break any of these rules sooner than say anything outright barbarous.
 



******************************
 

Nadhani,Mkuu, unachanganya mambo. Utajadilje yaliyomo kwenye kikombe kama kikombe chenyewe ni kichafu?

Watu hapa hatumpingi kuvaa kofia kageuza na miwani ya jua kila wakati. Tunachopinga ni kile tunachokiona kuwa ni/upretensious wa aliyevivaa. Huyu angesema anapiga muziki, baba yake ni milionea, anafanya kazi Google n.k. hakuna ambae angemstukia. Huyu anajiita social activist na investment banker. Kuthibitisha hilo imebandikwa piece ya kiuchumi ambayo inasemekana huyu investment banker ameiandika. Wengine tukiosoma hatuoni jipya ambalo limeandikwa. Tunaona ni article ya mtu kama Fundi Mchundo ambaye ni mpenzi wa magazeti ya ughaibuni. Magazeti kama Economist, Wall Street Journal, New York Times, The Guardian, International Herald Tribune n.k. Kusoma kwangu haya magazeti hata siku moja hakutanifanya mchumi mwenye uwezo wa kuandika a professional article on the subject. Ukijumuisha, what we unfortunately see as the shallowness of the article na uvaaji wa mwandishi ndiyo alarm bells zinazidi kupiga.

For too long, watu wanaoishi huko ughaibuni wametumia ukimya wetu na uoga wa kumkosoa mwenzetu kutuingiza mkenge. Kuanzia wale niliowataja walioanzisha timu za mpira mpaka hao waliotuuzia maturbine kanyaboya. Hii ni nchi ambayo mjanja aliwaingiza mjini wasomi wetu kwa ku/flash business card ya Pratt and Whitney na kusema yeye ni mwakilishi wao. Huyu mheshimiwa kaandika kitu katika public domain na ni haki akosolewe.

Sasa kudai kuwa tunafanya hivyo kwa sababu tunamuonea gele ni kupoteza mwelekeo. Gele ya nini? Kwa sababu anaishi ughaibuni? Wengi wa wanaomkosoa wanaishi huko huko. Kwa sababu ni kijana? Wengi wanaomkosoa nao ni vijana. Kwa sababu anafanya kazi nzuri( tunachojua ni mahali anapofanyia kazi lakini kazi anayoifanya hatuijui). Ameandika aricle ambayo hatuna uwezo wa kuiandika (ndiyo maana critic si mtendaji. Mgawanyo wa kazi).

mimi ningependa kuelewa kutoka kwa wale wanaomtetea, ni kitu gani alichoandika ambacho ni kigeni na kimelengwa kwa mtanzania? Au basi, ndiyo yale yale, ya ku-applaud mediocracy kwa sababu tu aliyeandika ni mwanetu? Hamumtendei haki. Kwa mtu makini angechukua hizi criticism to heart na kuzifanyia kazi ili baadae alete kitu ambacho wote tutampongeza. Kwa hii aliyoileta, safari yake bado ni ndefu.

Amandla......
 
kwikwikwikwikwikwi alikuwa anawanga, jamaa ana amini mambo ya ndumba. shauri lako, ukizidi kumfuatafuata atakushusha busha ndio ukome kuringa.

we wadhani hivyo.... pole sana.
 

Suala sio ugeni wa kitu bali relevancy yake kwa jamii.Kwa mfano,unaweza kuzungumzia HIV/AIDS ambayo ni tatizo lililokuwepo kwa miongo kadhaa,lakini japo si geni bado linahitaji attention ya jamii.Mbona takriban kila siku hapa JF tunazungumzia ufisadi japo si jambo geni?

Na kwanini achukue hizo criticism ili baadaye aje na kitu kinachostahili pongezi badala ya nyie critics kuja na kitu cha aina hiyo?Yeye ameonyesha njia (hata kama ina mapungufu kama inavyodaiwa),what about our critics?Na tayari kuna nafasi nzuri zaidi ya hapahapa kwenye topic hii!

At the end of the day,ni suala la mtizamo tu.Mwingine atasema mpira umetoka nje,mwingine atasema mpira umetoka ndani.Huyu atasema bilauri iko half empty,yule atasema half full.
 
Samahani mama, umekosea.
 

Fundi Mchundo is a beacon of reason.
 

Na mwingine atasema kama bilauri ni chafu there is little meaningful debate on that.
 

Haya, Mkuu. Nionyeshe kitu gani alichokiandika kina particular relevance kwa mtanzania?

Hao unaowaita critics wameishasema mapungufu wanayoyaona. Sasa badala ya kupinga walichokisema, unadai waandike ya kwao! Si critics wote ni waandishi. Ingekuwa hivyo basi watu wasingewachambua wachezaji wetu mahiri, waimbaji wetu, designers wetu, mafundi mchundo wetu n.k. Kwani makocha wote wanajua kucheza mpira kuliko wale wanaowafundisha?

Kwa mifano yako, mchezaji akiambiwa ametoa mpira nje kwa makosa basi jibu lake liwe basi njoo wewe ucheze! Au huyo mwenye bilauri akikosolewa, alivunje na kudai basi wewe uje na bilauri yako?

Criticism ni sehemu ya kukua. Kama unaogopa kukosolewa basi kaa nje ya public realm.
 


Fundi, baadhi ya watanzania hawapendi kukosolewa. Hii ni jadi, ukitaka kutest nenda mkosoe mmoja wa jamaa ukiwa na bahati mbaya utaona bifu lake, utaonekana si rafiki wa kweli na una wivu. Yaani rafiki kweli atakiwa awe mtu wa "ndiyo mzee", "hewala bwana", na "kumfagilia" tu hata kama unamfagilia kinafiki.

Hii imekolea sana huko serikali, na ndio inayozaa mitandao ya kijingajinga.

Usiulize kwa nini hatuendelei. Hatupendi challenge.
 
All I can say, Mjomba John M, inabidi ajitayatayarishie Uongozi tanzania kwa sababu kasi anayajadiliwa kwenye forum imevuka mpaka. amewakuna watu vichwa humu. Badala ya kujadili "contents" ya article yake, wameanza kumjadili binafsi na kuanza kutafuta mizengwe ya kumuaribia njia.

Huyu kijana ni mdogo sana, miaka 29 au 30 ni umri mdogo kulinganisha na vizee ambavyo vmeota siyo mvi bali kutu vichwani mwao ilhali hawajazifikia hatua alizopiga piga bwana mdogo.Tusubiri afikapo 40 kasi yenu itakuwa imefikia wapi, either way, ingekuwa vyema sana ikiwa baadhi yenu wangejaribu, badala ya kuandika pumba kwenye blogs, nanyi muandike essays hata moja moja kuhusu mada yake, ili tuone tofauti.

Lakini atakuwa amechemka tena sana kuacha kazi zake kwenda tanzania kwenye huo umri kupambana na well entrenched fisadis.

Endeleeni kumjadili lakini mjue kwamba mnavyozidi kumjadili ndio kadri mnavyozidi kumpatia umaarufu


Kwa wasiyo penda majungu, karibuni forum yenye utulivu

http://www.klhnews.com/
 

Kwa hiyo tukipenda "challenge" tutaendelea?
 


Fundi Mchundo mwenzangu,
Naona hujanielewa ninachotaka kusema hapa. Kumkosoa hata mie naunga mkono. Nimeandika kuwa nimekuwa na wasiwasi wa jamaa anavyotumia Internet kujitangaza. Ingawa ni hikihiki chombo Obama ametumia kushinda uchaguzi, kwa Tanzania bado sana. Angelirudi Tz na kuanzia kwenye roots kuonyesha jinsi alivyo mchapa kazi mzuri kwa mazingira ya Tanzania. You start from 0 hadi unaweka kitu kinachoeleweka.
Ukijadili na au ku-criticise artical yake mie sina matatizo. Ichambue vizuri tu na kuiweka kwenye vipande. Mie kinachonishangaza unapoanza hadi kujadili picha moja tu uliyoiona na haijulikani nani kaiweka hiyo picha. Hatujui hiyo ni artical yake ya ngapi. Hamjui alikuwa na ndoto ya miaka mingapi kuja kununua hiyo miwani na kofia. Alivyovipata akawa haachani navyo. Wengi tumepitia huko na tulikuwa na nywele zimefugwa na kukatwa ki-aina. Wengine walichonga mashati, wakakata suruali, wakazipanua kwa chini, wakavaa vi-stuli, wakaweka afro, waka...........
Mmoja hapa anasema kuwa ni kijana wa miaka 30. Ka utoto bado kamo ila anaweza kuwa na nia nzuri. Ni kumfundisha na si kum-KOMESHA. Naomba nitumie mfano wa Music producer Queens Jones. Huyu mzee nasikia sifa zake kubwa ukifanya naye kazi ni kuwa hata wewe Fundi Mchundo kama ukiandika wimbo ingawa milele hujawahi andika (tuseme), basi ukimpa ni kuwa siku zote jibu ni kuwa "ohhh, wimbo safi sana. Duu, wimbo mkali huuu....... ila unaonaje kama hapa tukibadilisha na pawe hivi, na pale hivi......." Mwisho wake unaweza kukuta kuwa ulichoandika kimebaki 10%. Ukweli utabaki kuwa huyu mzee na yeye hakukubaliana na wimbo wako ila amefanya hivyo kama ambavyo yule Tommy kwenye The Godfather anamwamba mtoto wa Don Carleon kuwa "jifunze kusema NO inayosound kama YES." Kumjadili Kiingereza chake, kofia yake, miwani yake, na sijui ingelionyesha meno basi hadi meno yake, simu yake, kiatu chake, shati lake nk kinaanza kutia wasiwasi, kweli hawa wanajadili hiyo makala yake au sasa wanamjadili mtu. Wangelijuwa hadi wazazi wake nao wangeliingizwa, maana mzazi wa mtu anayefanya kazi wall street hawezi akatia aibu.
Mama, wanasema msumeno hukata mbele na nyuma. Sasa unaposema kuwa wengine hawapendi kukosolewa, je wewe? By the way niliomba zile picha za matuta ya barabarani kwenye highway zetu. Sijui kama uliuona ujumbe.

Pundit, sijaona kama MIWANI na KOFIA ya jamaa ni chafu. Kama ni Kiingereza tumeambiwa Waingereza wenyewe wanafanya makosa. Ingelikuwa vema kumwelekeza kijana (ingawa sijui hata kama anasoma) na si kumkatisha tamaa. Nakumbuka wakati fulani kwenye Tanzanet ulizuka ubishi mkubwa sana juu ya Helcopiter isiyotumia mafuta. Tulibishana saana na mwisho akaja mwalimu kutoka UDSM idara ya Chemistry(Mr Rajab - heshima mbele) akasema imeandikwa "haitumii Fuel na si kuwa haitumii ENERGY". Ugomvi ukaisha. Ningelitamani mtu kama huyo aelezee sisi tunachopinga na kuwa kama KUMKOSOA kwa alichoandika basi hata sisi tunaunga mkono. Tukusoane na si KUKATISHANA TAMAA.
 


Criticism inakubalika, lakini inabidi ziwe na maana ndani yake. Jamaa amejadili Uchumi, chambua pointi zake kisha wote tutakubaliana ndiyo siyo mavazi yake. Kwani miwani itatuokoa kwenye janga la kiuchumi.umechangia nini kuhusu uchumi?


Unafahamu fika kwamba hili tatizo ni kubwa na linakuja kwa kasi, kila taifa linatafuta ufumbuzi, na ujuaji wako, nini umechangia, just answer that simple question realistically !
 

Queens who?
 

miaka 33, si mtoto mdogo, umaarufu si ndio anaoutafuta. Unadhani hakuna kijana wa miaka 28 anayefanya zaidi ya anayoyafanya huyo mjomba mjomba!
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…