Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 2,536
- 7,194
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) leo, Jumanne Machi 18.2025 kimemueleza Msajili wa Vyama vya Siasa kuhusiana na msimamo wake wa 'No Reform, No Election'
Akizungumza na wanahabari nje ya viunga vya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa muda mfupi baada ya kutoka kwenye ofisi hizo, Katibu Mkuu wa CHADEMA John Mnyika amesema viongozi wa chama hicho wamelazimika kufika kwenye ofisi hizo kufuatia wito walioupokea hivi karibuni
Kupitia kikao hicho kilichochukua zaidi ya saa nne, Mnyika amesema viongozi wa CHADEMA wameieleza Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini kuwa kauli hiyo hawajaitoa kwa bahati mbaya kwani kwa muda mrefu nchini kumeshuhudiwa chaguzi ambazo zisizokuwa huru na haki zisizoheshimu maoni ya wananchi wanayotoa kupitia masanduku ya kura, na kwamba mara zote imeelezwa na wadau mbalimbali kuwa mwarobaini wa yote hayo kufanyika kwa mageuzi ya mifumo ya uchaguzi ikiwemo kupatikana na Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi, jambo ambalo linaonekana kupigwa chenga na watawala (Serikali na CCM)
Soma Pia: CHADEMA wakiongozwa na John Mnyika waitikia wito wa kufika kwenye Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa
Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
"Sisi (CHADEMA) tunaamini baada ya kutuita na sisi kuitikia wito wao, sasa wanapaswa kuyachukulia kwa uzito ili na wao (Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa) wawe na mchango kama wadau wengine tuliokutananao, mchango wa kuwezesha kufanyika kwa mageuzi na mabadiliko kabla ya uchaguzi wa mwaka 2025, bila mabadiliko hakuna uchaguzi (No Reform, No Election) tunaamini jambo hili linapaswa kukubalika na wadau wote"
"Kwa hiyo katika hatua hii niwaombe tu vyombo vya habari badala ya kutuuliza kuhusu 'Tume' na yanayoendelea ya uandikishaji, kawaulizeni 'Tume ya Taifa ya Uchaguzi' ni kwa nini tangu mwezi Desemba hadi sasa hawajajibu barua yetu tuliyowaandikia ya kupata reform, sisi tumeshaweka msimamo bayana kwamba tunachokitaka kwa sasa ni mabadiliko ya Kikatiba na kisheria ya kuwezesha uchaguzi huru na haki kabla ya hatua nyingine zozote zinazohusiana na uchaguzi na tunataka wadau wengine wote watuelewe kwenye hili"