SI KWELI John Mnyika ajiuzulu nafasi ya Katibu Mkuu CHADEMA

SI KWELI John Mnyika ajiuzulu nafasi ya Katibu Mkuu CHADEMA

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Mbona mmekaa nayo kina John Mrema au hamtaki watanzania wajue...? Pole sana kamanda Mnyika ila nakupongeza kwa uamuzi huu muhimu na Mkubwa uliochokiamua ni ishara Tosha kuwa hukubaliani na wizi unaoendelea ndani ya Chadema

1724327388999.jpeg

 
Tunachokijua
John John Mnyika ni Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambaye mbali na nafasi ya ukatibu Mkuu wa CHADEMA pia amewahi kuwa mbunge wa Ubungo, mwaka 2010-2025.

images
Tarehe 22/08/2024 ilisambaa barua mtandaoni ambayo ilidaiwa kuwa ni ya CHADEMA ikiwa na ujumbe unaodai kuridhia ombi la John John Mnyika la kujiuzulu nafasi yake ya ukatibu Mkuu wa CHADEMA.

Barua hiyo inaeleza kuwa Mnyika ameamua kujiuzulu kutokana na wizi unaoendelea ndani ya chama cha CHADEMA na pia yeye Mnyika kunyimwa nafasi ya kusikilizwa mawazo yake ya kimaendeleo anayotoa ndani ya chama hicho, hivyo ameamua kujiudhuru na kwamba chama kimeridhia ombi lake. Unaweza kupata barua hiyo hapa na hapa.

Ukweli wake upoje?
Jamiicheck
imefuatilia Barua hiyo na kubaini kuwa ni barua iliyohaririwa na hajaandikwa na CHADEMA, katika kuzingatia hilo, barua hiyo haijawekwa kwenye vyanzo vyovyote vya habari vya cha hicho ikiwemo akaunti rasmi za CHADEMA wala hakuna taarifa yoyote kuhusu Mnyika Mnyika kujiuzulu.

Hata ivyo kupitia Akaunti rasmi ya Mtandao wa X, Mnyika hajazungumzia suala lolote kuhusu madai ya barua hiyo wala kuzungumzia suala la yeye kujiuzulu mpaka muda huu 14:00 wa tarehe 22/08/2024 ambapo bado utambulisho alioweka kwenye akaunti hiyo unasomeka kama Katibu Mkuu wa CHADEMA.

1724325780646-png.3076365
Pia, Jamiicheck Imezungumza na John Mrema, Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa CHADEMA, ambaye pia kwenye barua hiyo anaonekana kuwa ndiye aliyesaini, ambaye alikanusha jambo hili kwa kusema:-

"Ni taarifa za uongo na Upotoshaji, Katibu Mkuu Mnyika yupo ofisini na muda mchache alikuwa na Mwenyekiti Taifa Freeman Mbowe Mikocheni" mesema John Mrema.
Kwa akili Yako Mrema anaweza kuweka hizo sababu kuwa ndio zinamtoa Mnyika

Muwage na Akili bhana 😂
 
Mbona mmekaa nayo kina John Mrema au hamtaki watanzania wajue...? Pole sana kamanda Mnyika ila nakupongeza kwa uamuzi huu muhimu na Mkubwa uliochokiamua ni ishara Tosha kuwa hukubaliani na wizi unaoendelea ndani ya Chadema

Fisiem ,wakiona mambo yanawaendea vibaya na hasa , mambo ambayo Jamii inapaza sauti kwa wingi, basi wanatafuta jambo liltakalo ifanya Jamii Ku divert attention, ili wao wapumue.

Juzi sakata la Masai, lililo pamba moto, wakaghushi taarifa kwamba Tundu Lisu hakubaliani na Masai ya wamasai, wakijua sana kwamba Tundu Lisu ana ushawishi mkubwa kwa Watanzania, leo tena wanakuja na suala la Mnyika kujiuzulu, ni matapeli waandamizi hao
 
Back
Top Bottom