PreGE2025 John Mnyika: CHADEMA Tupo katikati ya Vita kubwa dhidi ya Watawala, njama zinafanyika kudhoofisha CHADEMA

PreGE2025 John Mnyika: CHADEMA Tupo katikati ya Vita kubwa dhidi ya Watawala, njama zinafanyika kudhoofisha CHADEMA

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Mnyika amesema chama hicho kiko katikati ya vita dhidi ya watawala, akidai kuna njama za kupinga uamuzi halali ya vikao vya chama na kujaribu kudhoofisha harakati za kudai mabadiliko ya kisiasa nchini.

Akizungumza leo Ijumaa, Mei 23, 2025, katika kikao maalumu chenye ajenda 12 kinachofanyika Makao Makuu ya Chadema, Mikocheni-Dar es Salaam, Mnyika amesema wakati huu ni wa kihistoria kwa chama hicho na Taifa, huku akikielezea kikao hicho kuwa sehemu ya kutafakari mustakabali wa Chadema na demokrasia nchini.

"Chama kinapitia wakati mgumu. Tupo katikati ya vita kubwa ya ‘No reforms, no election’ dhidi ya watawala ambao wanakwenda kinyume na matakwa ya wananchi."

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Amedai kuwa Serikali imekuwa ikipinga maamuzi halali ya Baraza Kuu la Chadema lililofanyika Januari 22, 2025, ambalo liliidhinisha uteuzi wa Katibu Mkuu, Naibu Katibu Mkuu na wajumbe wa Kamati Kuu.

"Watawala wanafanya kila jitihada kubatilisha maamuzi ya Kamati Kuu ambayo yalifanyika baada ya uongozi mpya kuingia madarakani. Hii ni vita ya wazi dhidi ya chama chetu."

Video: Mwananchi
 
Poleni sana 🐼

Njia iendayo mbinguni ni nyembamba tena imesongasonga sana na njia ya kuzimu ni pana sana tena imejaa mito ya vinywaji vya ulevi na muziki wa singeli

Kazi kwenu ufipa sasa mikocheni 😁
 
Wote walio wapigania haki na waliojotelea kwaajili ya watanzania maskini ni ndugu zangu
 
Mnyika aache porojo msajili kawaambie waitishe baraza muu ambalo litatimia akidi sio lao like feki lililowaweka madarakani ambalo akidi haikutimia kama katiba ya Chadema inavyotaka
 
Mnyika aache porojo msajili kawaambie waitishe baraza muu ambalo litatimia akidi sio lao like feki lililowaweka madarakani ambalo akidi haikutimia kama katiba ya Chadema inavyotaka
Wakati samia anajipitisha kuwa mgombea pekee wa urais kupitia fisiemu Katiba ilizingatiwa ?
 
Back
Top Bottom