John Mnyika: Kwa ukubwa wa mapito tuliyopitia Aprili 28-29 Kamati kuu itafanya kikao maalum

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), akizungumza na vyombo vya habari leo Jijini Dar es Salaam, John Mnyika ametangaza Kamati kuu ya chama hicho kufanya kikao maalum Aprili 28-29, 2026 ikiwa ni mara baada ya Mahakama ya Rufaa kuondoa zuio la chama hicho kutofanya shughuli ya siasa

Soma pia News Alert: - Mahakama ya rufani yairuhusu CHADEMA kuendelea na shughuli za kisiasa nchini

eo​
 
Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika, amesema kwa ukubwa wa mapito ambayo Chama hicho yameyapitia ya kuzuiwa kufanya shughuli za kisiasa kwa siku 310 na kwa majukumu ambayo yapo mbele yao anatangaza kwamba CHADEMA inaitisha kikao maalum cha Kamati Kuu haraka sana April 28 na April 29,2026 ambapo amewataka Wajumbe wa Kamati Kuu kusafiri kutoka maeneo mbalimbali ya nchi, wafike Makao Makuu ya Chama hicho Jijini Dar es salaam kuhudhuria vikao hivyo ambavyo vinafanyika kufuatia Mahakama ya Rufaa kuondoa zuio la Chama hicho kufanya shughuli za siasa kuanzia leo April 15,2026.

Akiongea Jijini Dar es salaam leo Mnyika amesema “Kwa ukubwa wa mapito tuliyopitia ya kuzuiwa kufanya shughuli za kisiasa kwa siku hizo 310 na kwa majukumu ambayo yapo mbele yetu nitangaze tu kwa nafasi ya Mtendaji Mkuu wa Chama kwamba tunaitisha kikao maalum cha Kamati Kuu haraka sana April 28 na April 29, 2026, Wajumbe wa Kamati Kuu wasafiri kutoka maeneo mbalimbali ya nchi, wafike Makao Makuu ya Chama ili tuwe na kikao maalum cha Kamati Kuu ya Chama”

“Na baada ya kikao hicho cha Kamati Kuu tutatafakari mambo mbalimbali ikiwamo uendeshaji wa Chama na yapo ambayo yatazungumzwa na Chama baada ya Kamati Kuu kukutana”
 
Police wanaweza kwenda kuzuia Mkutano, maana hili Talifa limekuwa la kambale, kila mtu ana ndevu.

Kila la kheri ndugu zetu wa CHADEMA.
 
Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika, amesema kwa ukubwa wa mapito ambayo Chama hicho yameyapitia ya kuzuiwa kufanya shughuli za kisiasa kwa siku 310 na kwa majukumu ambayo yapo mbele yao anatangaza kwamba CHADEMA inaitisha kikao maalum cha Kamati Kuu haraka sana April 28 na April 29,2026 ambapo amewataka Wajumbe wa Kamati Kuu kusafiri kutoka maeneo mbalimbali ya nchi, wafike Makao Makuu ya Chama hicho Jijini Dar es salaam kuhudhuria vikao hivyo ambavyo vinafanyika kufuatia Mahakama ya Rufaa kuondoa zuio la Chama hicho kufanya shughuli za siasa kuanzia leo April 15,2026.

Akiongea Jijini Dar es salaam leo Mnyika amesema “Kwa ukubwa wa mapito tuliyopitia ya kuzuiwa kufanya shughuli za kisiasa kwa siku hizo 310 na kwa majukumu ambayo yapo mbele yetu nitangaze tu kwa nafasi ya Mtendaji Mkuu wa Chama kwamba tunaitisha kikao maalum cha Kamati Kuu haraka sana April 28 na April 29, 2026, Wajumbe wa Kamati Kuu wasafiri kutoka maeneo mbalimbali ya nchi, wafike Makao Makuu ya Chama ili tuwe na kikao maalum cha Kamati Kuu ya Chama”

“Na baada ya kikao hicho cha Kamati Kuu tutatafakari mambo mbalimbali ikiwamo uendeshaji wa Chama na yapo ambayo yatazungumzwa na Chama baada ya Kamati Kuu kukutana”
kikao cha waropokaji waliopoteza uelekeo sio gentleman?
 
Wahuni na ripoti yao ya mauaji wajiandae kuchapwa ukweli unaouma mno
 
Sasa tutaona kama kweli alishindakwa asilimia 90
 
Back
Top Bottom