John Mnyika: Uchambuzi wa awali wa Ripoti ya CAG unaonesha tumepata hasara ya Trilioni 2

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2021
Posts
577
Reaction score
2,595
Akizungumza na wandishi wa habari makao makuu ya Chama cha CHADEMA muda huu, Katibu Mkuu wa Cha CHADEMA John Mnyika amesema bado wanaendelea kupiga hesabu ya hasara zilizotajwa na CAG, ambapo hadi sasa wamepata jumla ya Tsh. Trilioni 2.



Kuhusu DPP Biswalo Mganga, CHADEMA inashauri kiundwe chombo tofauti cha Kijaji ili kufanya uchunguzi na hatimaye kumchukulia hatua kwa kuwa tume ya Haki Jinai haina uwezo wa kumchukulia hatua yoyote.

Pia, amesema Rais hajatoa muda maalum wa Makatibu wakuu kujibu hoja za CAG, CHADEMA ina wasiwasi kuwa hoja hizo zinaweza kuchukua muda mrefu pasipo kupata majibu, hali ambayo hutokea kila mwaka. CHADEMA imeshauri Rais atumie vyombo vyake vya kimamlaka kuhakikisha hoja za CAG zinapata majibu kwa wakati.

Katika hatua nyingine, Mnyika ametoa wito kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuwajibika kwa kuwa yeye ndie msimamizi mkuu wa kazi za serikali, pia ni mtu anayewajibika na kufuatilia utekelezaji wa ripoti za CAG ambazo hazijafanyiwa kazi tangu ashike Wadhifa huo.
 
Ni hesabu za uongo. Vingine alivyotaja CAG siyo kupoteza hela bali ni kutokufuata taratibu
 
Ni hesabu za uongo. Vingine alivyotaja CAG siyo kupoteza hela bali ni kutokufuata taratibu
Ndio itajulikana baada ya uchunguzi. Huwezi kusema ni uongo au ni ukweli kabla ya Uchunguzi. Uchunguzi ndio utakaotoa majibu.
 
Ni hesabu za uongo. Vingine alivyotaja CAG siyo kupoteza hela bali ni kutokufuata taratibu
Usikimbilie kujibu kitu usichokielewa, hata ukiuza nyanya hasara hautaijua kizimbani, sasa wewe kabla haujamaliza kusoma umeshapata jibu eti kwa sababu tu ni mwanaccm uliye mafichoni! JF ni sehemu ya kujadili mambo ya msingi.
 
Hapo Kwa PM ndio patamo.
 
Chadema watu wa hovyo sana.

Wanachagua mtu wa kumwajibisha kwakua wameshalambishwa asali.

Hiki chama hakijawahi kuwa chama cha siasa bali wajasiliamali wa siasa.

Yeyote anayewalambisha asali wanamtukuza.
 
 

Attachments

  • 81D5E0D8-C6E9-4183-911D-F1910F380A27.jpeg
    112.6 KB · Views: 2
  • 31E63934-E041-43A2-AEB3-1EE8F4B12F47.jpeg
    121.5 KB · Views: 2
  • B3B5BA72-6A1A-4FFF-9D42-917C4794DFED.jpeg
    152 KB · Views: 3
  • D12F7698-1E1F-420B-BAEC-0C0CC1138381.jpeg
    149.6 KB · Views: 2
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…