Wabongo tatizo letu ndilo hili hili, kuangalia sana paper credentials na superficialities, ndiyo mana watu mpaka leo wanaongelea electability ya Kikwete kwa sababu ni so called "handsome" despite Nyerere kuwapiga shule.
Rais Harry S. Truman wa US hakuwa hata na college degree,lakini aliliongoza taifa lake vizuri, wakati wa vita nevertheless. John Major naye kaenda kuwa PM wa Uingereza bila ya college degree, leo hii mtu usipokuwa na degree naamini unakuwa disqualified, sasa tutawapata wapi kina Evo Morales wetu? Ina maana mtu mwenye enterpreneurial genius kama ya Bill Gates hawezi kuwa rais bongo kwa sababu tu hana degree, kunawengine wanaona degrees/ academics zinawapotezea muda tu, nao wasiwe na eligibility?
Swala muhimu hapa ni track record, Mnyika kafanya nini katika miaka yake ya kazi CHADEMA. Naamini mwenyewe ni member humu anaweza kuja na waraka wa kujibu kuhusu kazi.Vitu hujulikana uzuri wake kwa matokeo ya kazi, sio kwa paper qualifications ambazo mwenyewe ushaanza kuzikandya kwamba papers zinaleak.
Uki dispute/ tarnish matokeo ya form four kwamba paper zinaleak, basi inamaana hata kwa papers za form six paper si kigezo.
Let's focus on kazi, amefanya kazi gani? Haya mambo ya papers papers Tanzania kuna papers bwana? Papers zenyewe hazina standars wala syllabus, akija Mungai anabadili vyake akija Sitta anapangua hivi, kuna papers huko bongo zaidi ya kukomoana tu?
Ndiyo nyie nyie anakuja tapeli kavaa suti kubwa anaongea "kizungu" kigumu, ananukia uturi maridadi, mnamfungulia milango yote anaiba kila kitu.
Akija an ascetic intellectual shabbili dressed anayeweza kuwasaidia mnamfukuza. Kila kitu watu wanaangalia the superficial, wanaona the shallow bila kutaka kujua the deep.