Robert S Gulenga
JF-Expert Member
- Jan 3, 2013
- 2,255
- 1,565
Ndugu yangu John Mnyika, umekitumikia CHADEMA toka ukiwa Mwanachama wa kawaida, Mbunge hadi kuwa Katibu Mkuu wa Chama. Hakuna anayeweza kupinga kuwa muda wako mwingi umetumia kutetea Chama chako kwa nguvu zako zote na kwa uadilifu mkubwa kwenye chama chako.
John Mnyika, kwa namna ulivyo muumini wa siasa za kistarabu, siasa za kujenga hoja, siasa za kusikilizana, siasa za kukubaliana kutokubaliana, umekuwa Mwanafunzi mzuri wa Mh. Freeman Mbowe, kwa sasa Chadema si sehemu yako Sahihi, ni bora kwako kuachia nafasi ya Katibu Mkuu Chadema ukarudi CCM ili uendelee na siasa za kistarabu.
Najua sio rahisi kwa Mh. Freeman Mbowe kwa sasa kurudi CCM lakini muda utaamua, Mh Mbowe ni Muumini wa maendeleo na kwa sasa anaona namna Serikali ya Mh. Samia Suluhu Hassan inavyowaletea Watanzania maendeleo kwa kusogeza huduma muhimu karibu yao.
Ndugu yangu Mnyika, Makamanda wenzako Lema na Lissu hawataki kurudi Tanzania sio kwa sababu kuna tishio lolote kwa sasa bali wanaona Chama kimepoteza muelekeo, kimekuwa Chama cha kwenye mitandao, ukimya wa akina Msigwa ukupe hamu ya kurudi CCM, ukweli ni kwamba Watanzania wote asili yetu ni CCM na si jambo baya kurudi kwenye asili yako.
Maendeleo ni kwa Watanzania.
Mungu Ibariki Tanzania
Mungu Mbariki Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan.