John Mnyika wakabidhi chama chao, si dhambi kurudi CCM. Ukishindwa kabisa nenda kaungane na Zitto Kabwe kuendeleza Siasa za Upinzani

John Mnyika wakabidhi chama chao, si dhambi kurudi CCM. Ukishindwa kabisa nenda kaungane na Zitto Kabwe kuendeleza Siasa za Upinzani

Yaani unasema ccm ni chama Bora!Cha kistaarabu!!?
Kafulila yupo wapi?Ali happy,Malinda!!
Ni kweli jombaa hujapigiwa na katibu!
Wako Tanazania hapa hapa wanaendelea na utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi.
 
Ndugu yangu John Mnyika, umekitumikia CHADEMA toka ukiwa Mwanachama wa kawaida, Mbunge hadi kuwa Katibu Mkuu wa Chama. Hakuna anayeweza kupinga kuwa muda wako mwingi umetumia kutetea Chama chako kwa nguvu zako zote na kwa uadilifu mkubwa kwenye chama chako.

John Mnyika, kwa namna ulivyo muumini wa siasa za kistarabu, siasa za kujenga hoja, siasa za kusikilizana, siasa za kukubaliana kutokubaliana, umekuwa Mwanafunzi mzuri wa Mh. Freeman Mbowe, kwa sasa Chadema si sehemu yako Sahihi, ni bora kwako kuachia nafasi ya Katibu Mkuu Chadema ukarudi CCM ili uendelee na siasa za kistarabu.

Najua sio rahisi kwa Mh. Freeman Mbowe kwa sasa kurudi CCM lakini muda utaamua, Mh Mbowe ni Muumini wa maendeleo na kwa sasa anaona namna Serikali ya Mh. Samia Suluhu Hassan inavyowaletea Watanzania maendeleo kwa kusogeza huduma muhimu karibu yao.

Ndugu yangu Mnyika, Makamanda wenzako Lema na Lissu hawataki kurudi Tanzania sio kwa sababu kuna tishio lolote kwa sasa bali wanaona Chama kimepoteza muelekeo, kimekuwa Chama cha kwenye mitandao, ukimya wa akina Msigwa ukupe hamu ya kurudi CCM, ukweli ni kwamba Watanzania wote asili yetu ni CCM na si jambo baya kurudi kwenye asili yako.

Maendeleo ni kwa Watanzania.

Mungu Ibariki Tanzania

Mungu Mbariki Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan.
JF imevamiwa na maadui wa demokrasia. Kile chama cha wauaji na watekaji. Wanajiita wastaarabu!!!
Kile chama kilichozamisha binadamu wenzao baharini ndani ya viroba eti wastaarabu. Mashetani wanataka kukaribisha malaika motoni. Kama wewe ni binadamu basi ni msukule
 
Mkuu nani ni adui wa Demokrasia? kungekuwa hakuna demokrasia unadhani ungepata muda wa kuita watu mashetani, wauaji na ukawa huru? Demokrasia iliyopo ndiyo inayofanya uwe huru hivi,
Mungu Ibariki Tanzania na Watu wake.
 
Kubali too hata Tulia juzi alizindua shughuli ya uuaji kwa kutumia UVCCM kwa wapinzani. Ustaarabu!!!!
 
Hayo maneno ya kila siku ambayo hayana hata ukweli, hakuna mwaka Wapinzani wamewahi kukubali kushindwa duniani kote
Wale walioenguliwa kwa visingizio walipigiwa kura???Sijawahi ona nchi yoyote yenye demokrasia mtu au mgombea anapita bila kupingwa hili halipo kabisa labda Rwanda,Burundi na DRC.
 
Mi napita tu lakini ilikuwa si rahisi kupita siku au hata saa bila kuona jitihada za mwenzetu erythrocyte katika kujaribu kuwaaminisha watu kuwa chadema ipo kwa nyuzi mbalimbali......lkn sasa nahisi ameshajichokea, si kwa kimya hiki. Wapo 'makamanda' wachache wanajaribu lakini mh!!
 
Hakuna kitu kigumu kama kutetea chama kilichopoteza mvuto kwa Wananchi NIMEONA
 
Back
Top Bottom