John Heche ni mwanasiasa kutokea nchini Tanzania, ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti bara wa chama cha demokrasia na maendeleo (
CHADEMA). Wakati
John Mrema akiwa ni mwanasiasa pia kutokea Tanzania ambaye amewahi pia kuwa kiongozi na mwanachama wa CHADEMA kabla ya kuhamia chama cha ukombozi wa Umma (
CHAUMMA) ambapo anahudumu kama Mkurugenzi wa mawasiliano.
Madai
Kumekuwapo na Poster inayosambaa katika mitandao mbalimbali ya kijamii ikiwa na utambulisho wa Jambo TV ikiwa na ujumbe unaoeleza
"HECHE ANASHIKILIWA KWA KUBEBA MIRUNGI". Poster hiyo pia iliambatana na inayoonekana kuwa ni screenshot ya ujumbe wa John Mrema kutoka katika ukurasa wake wa X (twitter).
Uhalisia wa madai hayo ni upi?
Ufuatiliaji uliofanywa na JamiiCheck umejirirdhisha kuwa madai hayo si ya kweli. Ufuatiliaji kwa njia ya mtandao umebaini kuwa screenshot inayoonekana kuwa ni ya John Mrema akitoa tuhuma hizo kupitia ukurasa wake wa X, si ya kweli.
Taarifa hiyo ilisambaa ikionekana John Mrema alichapisha taarifa hiyo Oktoba 23, lakini ufuatiliaji ulibaini kuwa John Mrema kwa mara ya mwisho alichapisha katika ukurasa wake wa X
ilikuwa ni Agosti 18. Ujumbe wake wa mwisho ulisomeka;
"CHAUMMA,yamwandikia barua waziri wa Mambonya ndani kuhusu wananchi wa Liwale kunyanganywa mifugo yao na kutakiwa kulipa faini kwa Polisi."
Sambamba na hayo Poster inayoonekana kuwa na utambulisho wa chombo cha habari cha
Jambo TV ni ya kubuni na haijachapishwa na chanzo hicho.