Mwande na Mndewa
JF-Expert Member
- Feb 26, 2021
- 1,322
- 3,648
Kila Rais atakayekuja kuongoza nchi hii atakutana na changamoto kubwa sana.atapimwa kwa kiwango cha juu je, ana uwezo wa kuvaa viatu vya Hayati Dkt. John Pombe Magufuli?
Mambo aliyoyafanya wakati wa uongozi wake ni vigumu mno kusahaulika au kufutika katika fikra na mioyo ya Watanzania.
Alikuwa kiongozi wa kipekee mwenye uthubutu, mzalendo wa kweli, na mtendaji asiyeogopa changamoto alisimama kidete kwa ajili ya maslahi ya taifa, akapambana na ufisadi, uzembe na matumizi mabaya ya rasilimali za umma.
Kuna msemo usemao nyayo za tembo hazifutwi kwa ufagio.
Uongozi wa Magufuli umeacha alama kubwa alama ambazo zitabaki kuwa kipimo kwa kila anayekuja.
Kila kiongozi mpya atalinganishwa naye, kwa sababu aliweka viwango vya juu katika utendaji na uwajibikaji.