John Wick 2014 haina simulizi inayoeleweka! Storyline yake ni mbovu!

John Wick 2014 haina simulizi inayoeleweka! Storyline yake ni mbovu!

Cecil J

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2023
Posts
434
Reaction score
1,024
Awali ya yote kwa yeyote aliyekuja pupa ili kunijibu nina maneno mawili tu, "Punguza spidi", rejea kichwa cha uzi kisome vizuri kisha urejee tena.

Nakiri kwamba sikuwahi kuangalia filamu ya John Wick hapo awali, nilikutana na Posters zake tu ila sikupata muda wa kuitazama.

Siku ya juzi nimejipa muda na kuzitafuta hizi filamu za John Wick, nilizipata nne: John Wick 2014, John Wick 2017, John Wick 2019, na John Wick 2023.

Nikaanza rasmi kuitazama John Wick 2014, muvi ilikuwa na Quality kali kidogo (720p) na niliangalizia kwenye PC angalau nisikose baadhi ya vitu.

Filamu imeanza John Wick amefiwa na mkewe, hapo nikaona sawa simulizi inaendelea. Sijakaa sawa jamaa-J.Wick ameanza kukaa na mbwa. Siku kadhaa aliingia barabarani (ikiwa ni siku chache tangu alipopatwa na msiba wa mkewe) na kutembeza gari yake.

John Wick akiwa stesheni ya mafuta anakutana na vijana riff raff wanamkoromea kihuni na kuondoka, imefika usiku wanamvamia na kumpiga na iron bat na kuiua mbwa yake. Nilijua kuna kitu kingine kitaendelea nashangaa eti hapo star mwenyewe-J.WICK ameshapaniki tayari anakimbilia mitutu then baba wa aliyewaongoza wenzie kumvamia J.WiCK anaanza kuimba mapambio ya kumsifia J.WICK.

Sijakaa sawa tayari saa 1 na dakika 41 zimeisha.

Nimejuta kuiangalia hii filamu!
 
Ndio. Na ni kitu relatable, mbona kuna watu tunajisikia hivyo?
Sawa inawezekana hakuwa vizuri kisaikolojia baada ya kumpoteza mkewe. Ila matukio ya ile muvi yapo hovyo sana, saa 1 na dakika 41 ni muda mrefu na unafaa kuweka matukio yanahotakiwa na yasiyotakiwa. Mbona wameunganisha vitu visivyo na umuhimu?

John Wick kuenda ile sehemu inayofanana na Airport ku-drift gari hakukuwa na maana. Kama lengo ilikuwa azinguliwe na wale madogo basi tukio lingetafutiwa angle nzuri na sio kupachika tu!
 
Ni non-linear storytelling, mbona filamu nyingi zinafanya tu...

Tena filamu kubwa kama inception
Muvi iliyokaa kwa mtu mmoja ina mpangilio wake, sijasomea masuala ya muvi ila namna ya upangaji wa matukio ina athiri hata utazamaji.

Bora niirejee sisu ila sio hii John Wick 2014 na dada yake John Wick 2017
 
Sawa inawezekana hakuwa vizuri kisaikolojia baada ya kumpoteza mkewe. Ila matukio ya ile muvi yapo hovyo sana, saa 1 na dakika 41 ni muda mrefu na unafaa kuweka matukio yanahotakiwa na yasiyotakiwa. Mbona wameunganisha vitu visivyo na umuhimu?

John Wick kuenda ile sehemu inayofanana na Airport ku-drift gari hakukuwa na maana. Kama lengo ilikuwa azinguliwe na wale madogo basi tukio lingetafutiwa angle nzuri na sio kupachika tu!
Alidrift kwasababu analipenda lile gari. Ana mahusiano nalo.
 
Dah!
Umewahi tazama series au muvi yoyote yenye stori iliyotulia? Mfano series za Merlin, Mindhunters, na zingine zinazoendana na hizo?
kuhusu stori kuvutia ni suala la kimtazamo sana

ila kwenye john wick kuna mambo mengi ya kizungu yamewekwa pale, mfano mtu kupenda gari, ambayo wengi hatutaki kuyaelewa
 
kuhusu stori kuvutia ni suala la kimtazamo sana

ila kwenye john wick kuna mambo mengi ya kizungu yamewekwa pale, mfano mtu kupenda gari, ambayo wengi hatutaki kuyaelewa
J.WICK ana over-obsession ya gari hilo sikatai. Shida ipo kwenye mpangilio wa matukio ni hovyo mno, yaani ukiambiwa uorodheshe matukio makubwa ni matatu tu: Kufa kwa mke wa John, Kuvamiwa na kuuawa kwa mbwa wa John, na mwisho ni John Wick kuwa wild na kuuwa watu basi.
 
Simple.

Halafu kule wameleta utofauti kwenye genre ya assassins, kuna sheria za ajabu ajabu

Action scenes ziko vizuri pia
 
Back
Top Bottom