Johnson Mashaka na mbio za Ubunge Ukonga

Johnson Mashaka na mbio za Ubunge Ukonga

Muke Ya Muzungu

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2009
Posts
3,444
Reaction score
265
Vyanzo vyetu jijini Dar es salaam, vimethibitisha hali isiyo ya kawaida ambapo , Mwanaharakati John Mashaka amelivamia na kuliteka jimbo la UKONGA. Bw. John Mashaka ambaye yupo nchini kwa likizo, ameingiza magari matano, aina ya Landruiser 4X4 pamoja na kuweka kitita cha Dola za kimarekani karibia $350,000 kwa ajili ya kampeni yake. Hizi habari zimevuja kutoka ndani ya kamati ya kampeni

Bw. Mashaka, ameunda timu yake ya kutisha, ambayo imeundwa na wasomi kadhaa toka chuo kikuu cha Dar es salaam pamoja na wazungu Fulani wanaosadikiwa kuwa wamarekani ambao kwa pamoja wataendesha kampeni yak e kupitia Chama Cha Mapinduzi. Vile vile Bw. Mashaka ameonekana na hawa wazungu watatu ndani ya moja ya hayo magari yenye “tinted windows” katika kata ya Kinyerezi wakiongea na wananchi.

Kilichomtia Bw. John Mashaka jeuri ni uwezo wake wa kifedha na pia , kundi lake likiongozwa na mhadhiri mmoja “jina kapuni” kutoka chuo kikuu cha Dar, ilifanya utafiti wa siri kwa kipindi cha miezi sita na kugundua kwamba, kati ya wapiga kura 10 waliohojiwa jimboni kote, 7 hawatampigia kura tena Bw. Makongoro Mahanga, kutokana na kinachodaiwa kwamba Bw. Mahanga alitoa ahadi ambazo hazikutekelezaka.Vile vile Bw. Mashaka anasukumwa na wanasiasa wazito kutoka Chama tawala ambao wanamuona kama nyota chipukizi ambaye ataliokoa chama tawala, hasa kutoka katika kashfa ya ufisadi.

Habari hizi nyeti zimemfikia mbunge wa sasa wa Ukonga Mh. Milton Makongoro Mahanga ambaye ambaye ameingiwa na hofu kubwa na kulazimika kufanya kazi usiku na mchana ili kutetea jimbo lake hasa baada ya kusikia mambo ambayo Bw. Mashaka ameyafanya katika jimbo lake, hususan kumwaga karibia nusu Billioni na kutayarisha kamati yake ya kampeni inayotisha. Wiki iliyopita walionekana maeneo ya Ubungo plaza wanakofanyia vikao vyao

Ndugu wadau, kama kweli John Mashaka amejikita ulingoni, basi chachu mpya hasa ya mabadiliko nchini Tanzania imeanza kwa sababu uwezo wa huyu mtoto ni wa aina yake, kwa maana hiyo pamoja na Zitto Kabwe ambaye yuko upinzani, Chama tawala itakuwa na kichwa na kijana mwenye kipaji cha aina yake. Jimboni Ubungo nako yupo Nape Nauaye , Temeke January Makamba. Kwa maana hiyo Dar Es Salaam itachukuliwa na vijana. Swahiba wa John Mashaka, Dr. H Shayo wa Kule London naye yuko njiani kuelekea Moshi kwenye Kampeni

Je wadau, hii imekaaje? Hawa vijana watatu Mashaka, Shayo,na January ni Chachu mpya au nguvu ya Soda tu? Kama kweli watajitosa ulingoni, basi sura ya Tanzania itabadilika, kwa sababu uwezo wa kubadilisha nchi wanayo na ni majasiri kupambana na ufisadi, na nina uhakika Rais 2015 atakuwa mmoja wa hawa vijana watatu kama siyo Membe

Bila kusahau, ndugu yetu mwanakijiji vipi yeye anagombea wapi?
Tutawapa taarifa zaidi pale tutakapozipata…………………! Endeleeni kukaa mkao wa kula

UPDATE 1:

Hotuba ya John Mashaka:

HOTUBA YA JOHN MASHAKA KATIKA
VIWANJA VYA BIAFRA, KINONDONI

Mheshimiwa Profesa David Mwakyusa, Waziri wa Afya na ustawi wa Jamii, wadhamini wetu kampuni ya zain, clouds FM na Business Times, wageni waalikwa na watanzania wenzangu.

shukrani za dhati kwa kuukubali huu mwaliko, na kujumika nasi wa siku ya leo kujikumbushia maswala muhimu kuhusu taifa letu hasa maswaa ya haki na usawa. Huu ni uzalendo wa aina yake, ni uzalendo unaotukumbushia uhuru wetu wa mwaka 1961, nchi hii iliposaini hati ya makabidhiano ya uhuru,

Hati ya mwaka 61 iliikabidhi nchi yetu haki yake ya msingi, haki ya maamuzi yaliyo mhakikishia kila raia maisha bora, na usawa. Hati hiyo ya mwaka 1961, ilitoa matumaini kwa kila mmoja. Raia wa Tanzania, walihaidiwa maendeleo makubwa.Watanzana hawakuahidiwa haya yanayojitokeza kwa sasa ; hawakuhaidiwa ahadi zisizotekelezeka, Walipewa ahadi za dhati za kukabiliana na maradhi, ahadi za kuondokana na umasikini na ujinga. Watanzania walipewa ahadi za haki, bila kujali matabaka, walihaidiwa usalama kwa raia wote.

Ahadi za mwaka 1961 hazikuwa za kuleta ufisadi kama huu tunao ushuhudia sasa. Hati ya Uhuru ilikuwa ni ya manufaa kwa raia wote. Kwa hakika katika miaka 48 ya uhuru wetu, yapo mambo kadhaa ya kujivunia.


Kuna mabadiliko makubwa hasa katika jiji la Dar es Salaam na hata kwingineko Ambako Kuna majengo marefu, mazuri ya kisasa, yanayoelekea mawinguni. Miaka 48 imeleta mabadiliko ya kijamii, kuna matabaka ya wasomi wenye maisha ya juu. Kuna makundi ya watawala na wenye mamlaka; Kuna kundi la matajiri wanaoshi katika sayari tofauti na watanzania walio wengi.

Watanzania wenzangu, wakati wapo wenye maisha mazuri, wanaoishi katika raha na utukufu, wapo pia wengi ambao wana maisha ya dhiki, wapo mamillioni wanaoshi katika ukiwa. Wapo wengi wanaoishi kwa kubahatisha na kwa kukata tamaa; wale ambao hawaoni faida waliyoitegemea kutokana na kupatikana kwa uhuru wao. Wapo maalbino wanaoishi kwa ukiwa na wasiwasi mkubwa.

Umbali mfupi tu kutoka hapa tulipo wapo wenzetu ambao wanaishi kwa hofu; wanaume kwa wanawake walio na wasiwasi, siyo tu juu ya maisha yao wenyewe, bali maisha ya umbele ya kiafya, na kielimu kwa watoto wao.Hawa ni raia wenye hofu kuhusu usalama wao. Ni raia wenye hofu jinsi watakavyowalisha watoto wao.Ni raia wenye wasiwasi ni jinsi gani watawasomesha watoto wao, siyo katika shule za ng’ambo bali katika shule za humu nchini. Hawa ni raia wenye hofu ya kupata hata mmlo mmoja kwa familia zao nahuu ndio ukweli wa mambo; Ni ukweli unaouma.

Ukweli wa mambo wenye machungu,haupo mbali nasi, ukweli huu upo manzese, upo kigogo na kule Temeke. Hali mbaya zaidi ya ukweli huu upo pale msimbazi center ambapo vitoto vichanga vya miezi mitatu vinaishi kwa uwezo wa mwenyezi Mungu ili hali nchi yao inayo uwezo wa kuwapa maisha yenye uhakika. Ukweli unaosononesha tunao hapa kati yetu, ambapo maelfu ya vijana hawana ajira, ni wachovu katika lindi la ufukara. Ukweli huu unaoumiza tunauona kwa vijana wetu ambao, licha ya kuwa wamesoma vya kutosha, wanabakia wakichuuza maji ya kunywa ili kujikidhi kimaisha.

Wengine wanaamua kuchukua silaha na kufikia hatua ya kuyachukua maisha ya wengine ili kujipatia riziki. Huu dio ukweli wa mambo; ni ukweli unaouma.

Natumia nafasi hii kuwasihi wale wote wanaochota raslimali za inchi hii; Wale wote ambao wanahamisha mamilioni ya pesa za walipa kodi na kuyapeleka katika akaunti nje ya nchi, Nawasihi wale wote wenye roho za kifisadi kufikiria mara mbili juu ya maadili na vitendo vyao.

Nawasihi hawa waliopewa dhamani ya kuilinda hii nchi kuvitembelea vyuo vyetu, na tasisi nyingine za elimu ili kuangalia hali halisi ya mahitaji katika taasisi hizo. Nawasihi viongozi wetu kwenda katika vituo vya mabasi, na masokoni na kuwaona vijana na watoto wadogo waliolemewa na ufukara, wanaolala kwenye mabaraza ya majumba na kwenye magenge kwa sababu hawana makazi. Nawasihi viongozi wetu kutega masikio yao ili kuwasikia, vijana wenye majonzi makubwa , vijana wanozishuhudia ndoto zao za kielimu zikitokomea kutokana na ufukara mkubwa walionao wazazi wao.

Siku ya leo ndugu zangu, tunawaomba viongozi wetu wavisikie sauti za ndugu zetu wanaowindwa kutokana na uumbaji wa Mwenyezi mungu. Tunawaomba wazisikie sauti za ndugu zetu maalbino wanaoishi kwa uwoga na ukiwa . Tunaomba walindwe, na kupewa haki zao za kimsingi, na za Usalama. Hii siyo tu kwao maalbino, bali kwao watanzania wote wanaotikiswa na wimbi la ujambazi. Hii siyo hati nchi yetu ilisaini kwa ajili ya raia wake, Hii ni hundi batili MAFISADI wa kimaadili wanawalazimisha raia wema kuvichukua.

Tunawasihi viongozi wetu waondoke nje ya ofisi zao ili watafute muhafaka kwa kushirikiana na wananchi wengine juu ya ulinzi wa watoto albino wasio na hatia. Ninawasihi, msikie kilio cha yule Albino, binti wa miaka 10 ambaye hawezi kukilalia kitanda kimoja kila siku kwa sababu tu anawindwa na watu wenye tamaa na imani potofu. Huu ndiyo ukweli wa mambo, ukweli wa miaka 48 ya uhuru wetu!

Ni ukweli unaouma !

“Miezi michache iliyopita nilighafirika kwamba kiongozi mmoja wa ngazi ya juu wa Kimarekani niliyeongea naye, aliweza kuikumbuka Tanzania kwa mauaji ya albino badala ya mambo mengine mengi mazuri tu yanayoihusu Tanzania”.Jambo hili ni la kifedheha! Huu ni umaskini wa kifikra na UFISADI wa kimaadili ambao umetukumba sisi watanzania. Kumuwinda binadamu kutokana na umbile lake siyo utanzania, huu ni ushetani.

Tusiitegemee serikali kuwa na miujiza ya kusuluhisha kila tatizo letu la kijamii na kiusalama. Tatizo hili lipo mikononi mwetu. Sisi raia ndio wenye nguvu na uwezo wa kutokomeza haya mauaji ya kinyama. ni lazima tushirikiane ili kuzuia jambo hili la kiovu. Watanzania wenzangu, wakati wapo wenzetu wanaume kwa wanawake chini ya bahari, angani na kwingineko wakifanya utafiti na shughuli zenye hatari kubwa kwa manufaa yetu, nchini kwetu, wengine wanatafiti namna ya kuwaua maalbino wasiokuwa na hatia. Tuwalindeni maalbino, tuwasaidieni tunapoweza.

Ndugu zangu, tusipojitizama vizuri, basi tunakokwenda ni giza kubwa na majonzi yasiyokuwa na kipimo kwa sababu binadamu ambaye hawezi kuyathamini maisha hana zaidi ya kuthamini.

Tumeumbwa tulindane, si kuwindana.
Tumeumbwa kuwa watumishi, siyo watumikiwa,
Tumeumbwa kuwatendea haki wanyonge, siyo kuwanyanyasa,
Tumeumbwa kujitolea kwa hali na mali kwa manufaa ya wengine.

Hiyo ndiyo maana halisi ya maadili, Hiyo ndiyo maana ya uongozi!
Mwanafalsafa wa Kimarekani , Edmund Burk, alipata kusema kwamba, “ tofauti kubwa kati ya kiongozi wa dhati na yule ajifanyaye kuwa kiongozi ni kwamba; kiongozi wa dhati uangalia mbele, wakati yule bandia uangalia ya leo. Kiongozi bandia anaishi kwa ajili ya leo na anatenda udanganyifu, wakati mwenzake anavumilia machungu ili kuyalinda madili na kutizama maisha ya baadae”.

Viongozi wanaoipenda hii nchi, badala ya kutafuta utajiri wa kitambo, tunawaomba muangalie ni wapi tunaelekea. Tunawaomba mtafakari mustakabali wa nchi na maisha ya mbeleni ya vijukuu vyenu ambavyo havitahitaji mabillioni ya fedha ya wizi iliyolimbikizwa nchi za nje. Bali mazingira mazuri ya kuishi yenye amani .

Ndugu zangu, muda hauna uhadilifu wala subira. Muda hauwezi kubadilisha au kutatua matatizo yetu, Muda hauwezi kuponya vindonda vilivyosababishwa na umasikini. Muda hauwezi kuyarudisha maisha yaliyopotezwa kutokana na tamaa na ulafi wetu. Muda haupo upande wetu, wala maneno matupu hayawezi kuponya maumivu.Muda hauwezi kutuondoa katika masumbuko yetu, bali unaweza kutuacha ili tuendelee kuumia.

Wakati umefika tujitoe mhanga ili kuleta mabadiliko na kuondokana na maumivu yanayotukabili. Wapo wengi ambao wamekuwa wakihoji haya ninayoyafanya katika jamii, wengine wamekuwa wakidhania kwamba nina malengo ya kisiasa !

Ninachoweza kusema ni kwamba mtu yeyote mwenye hutu ambaye analiona wingu la umasikini uliotanda katika taifa letu, anayo jukumu la kimaadili kutoa mchango wake ili kuondoa kukata tamaa kunakowakabili mamilioni ya wanachi wetu, dhamira hii ipo juu ya dhamira nyepesi za kisiasa.

Ninalilipa deni langu kwa jamii yangu. Nalipa fadhila kwa mwenyezi Mungu. Haraka iliyopo katika hitaji la kuwasaidia ndugu zetu wenye matatizo, ni ya kasi zaidi kuliko haraka ya kukimbilia madaraka ya kisiasa. Hitaji la kumsaidia mtoto mwenye kulala na njaa ni kubwa kuliko tamaa za madaraka ya kawaida ya kisiasa.

Kimsingi huo ndio mvuto mkubwa ambao umekuwa ukiusumbua nafsi yangu kwa muda mrefu. Ninachokifanya ni sehemu tu ya utashi wa kiroho ambao umenifunulia wajibu wangu, na jukumu langu kama binadamu mwingine anayetambua kati ya wema na uovu. Huu ni utashi ulionipa changamoto ya kujitazama upya katika taswira ya maadili. Ni utashi unaotusihi wote kujitolea mhanga kwa ajili ya amani katika taifa letu.

Kila mmoja ana ndoto ya kuishi maisha yenye furaha. Wote mliopo hapa mmekuja kwa sababu mnaamini kwamba tunalindwa na bendera moja, na kutumikiwa na rais mmoja. Hivyo, nawasihi mrudi majumbani kwenu na ujumbe mmoja kwamba, maisha yenye matumaini ni muhimu kuliko maisha ya kukata tamaa.

Ni lazima wote tufahamu kwamba upendo ni muhimu kuliko chuki. Lazima mtambue kwamba ushirikiano ni muhimu kuliko utengano. Hizi ni tunu ambazo tunatakiwa kuzilinda; Ni lazima tuwe sehemu ya mabadiliko kueleka katika maendeleo chanya.

Kufika kwenu hapa leo imekuwa kama chanzo cha uharakati wa watanzania, uharakati wa kijamii ya kuwalinda wenye ulemeavu, wenye ukoma, na wasioona. Ni uharakati wa kuwavalisha wanaotembea uchi. Ni uharakati wa kuwalisha wanaoshinda njaa. Ni uharakati wa kuwalinda maalbino wanaoishi kwa wasiwasi na ukiwa

Ni uharakati na maendeleo ambayo yamevuka mipaka ya siasa, dini, hata asili za watu. Ni maendelao yaliyovuka ubaguzi wa rangi, matabaka, na hata kasumba. Ni maendeleo yanayowakutanisha Watanzania wote. Huu ni uharakati na mchakato wa masikini na matajiri. Mchakato wa wenye madaraka na wanyonge, Ni mchakato kuhakikisha kwamba MAFISADI na masikini wanapewa haki sawa mbele ya sheria.

Ni mchakato na uharakati wa kuleta upendo kwa kila mwanadamu. Ni mchakatona ambao umedhamiria kurudisha yale matumaini ambayo watu walikuwa nayo mwaka 1961 wakati nchi yetu ilipopata uhuru. Uharakati wa kuondokana na magonjwa, ujinga, na umasikini. Uharakati wa kuhakikisha usalama kwa kila raia. Uharakati wa kukomeza Ufisadi.

Haya ni mapambano ya kuwalinda watu wote bila kuwabagua,
Ni mapambano ya kuwalinda maalbino.
Ni mapambano yaliyaonza mwaka 1961;
Ni mapambano yenye manufaa kwa kila mmoja wetu.

Mungu Ibariki Tanzania
 
Mmeanza yenu ya kuchafua vijana kwa visingizio vya pesa na madudu mengine.

Eti dola 350,000 ni propaganda tu, wewe umeziona hizo pesa?

Huwezi kufanya breaking news kitu ambacho huna uhakika nacho.
 
Tupe chanzo cha habari yako. Magazeti ya udaku ndio huwa na vyanzo visivyo julikana. Je huu pia ni udaku?
 
Tatizo kama hau wadau wapo CCM basi hawana jipya watakaloliweza kulifanya ili kuiendeleza nchi hii ,wengi sana waliingia katika siasa wakiwa na roho na mioyo mikunjufu kabisa lakini ugonjwa uliomo ndani ya CCM ni wa kuambukiza ,hivyo kasi zao zitaishia kwenye mwongo wa mwanzo tu pengine hata zisionekane tena,na hao mazungu isije kuwa ni rasilimali wameekeza kwa huyo mbongo,na baadae watahitajia kulipwa kwa kupewa maeneo wafanye watakalo.Na pangu pakavu wahamishwe kwa mtutu wa bunduki.
 
Kama Mashaka atatumia kiasi cha fedha kilichotajwa kuhonga wapiga kura basi hana tofauti na mafisadi wengine. Hata tukikubali kuwa fedha ni kwa ajili ya kampeni, je Mashaka ni mjinga kiasi gani atumie kiasi kilichotajwa bila kutegemea kupata faida zaidi ya fedha aliyoitumia?
 
Ahahah!, Uwanja wa Porojo...Kweli Politics ni Dirty Game!...

Mmeanza kumchafulia Mapemaaa, Hii Ni Ishara ya WOGA! Kama Mbwa Koko,

B.
 
John Mashaka anatafuta kujiabisha tu . Kwanza zengwe pili atafunikwa akasemee kwenye Chama.CCM imezoea dhuluma hata aje nani ndani hawezi kubadilisha. Eti January Makamba . Huyu dogo si yuko Ikulu hata mail address hakuna ama uwezo wake utaanza kuonekana akiwa Bungeni huko Temeke ? Masikio hayazidi kichwa baba ana babwaja huo umakini wa kijana ni upi ? Nape ni opportunist hanisumbui kabisa . CCM ni ndoto bwana . Wazungu hao kama wako na mission ndiyo wao wnataka kumtumia kufanya biashara tu .Na Mashaka anakuja na mapesa ufisadi kabla hajaanza .
 
Bw. John Mashaka, kwa ushauri wangu, nadhani usiingilie sisasa kabisa. Heshima uliyonayo katika jamii inatosha. uwezo wako wa kibusara na kifedha unatosha, usiingie kwenye siasa. watakumaliza, watu kama wewe hawachelewi kutolewa nje.

Waachie wakina makongoro mahanga waendeleze libeneke lao la dirty politics. hata kama una nia, umri wako bado mdogo, subiri 2015 uwe rais moja kwa moja. ila Subiri Nyani Ngabu na Julious waamke wana majungu ambao kazi yao siku zote ni kuwaponda wengine, niaminie watashambulia kweli hizo hela ulizotoa.
 
Ndugu wadau, kama kweli John Mashaka amejikita ulingoni, basi chachu mpya hasa ya mabadiliko nchini Tanzania imeanza kwa sababu uwezo wa huyu mtoto ni wa aina yake, kwa maana hiyo pamoja na Zitto Kabwe ambaye yuko upinzani, Chama tawala itakuwa na kichwa na kijana mwenye kipaji cha aina yake. Jimboni Ubungo nako yupo Nape Nauaye , Temeke January Makamba. Kwa maana hiyo Dar Es Salaam itachukuliwa na vijana. Swahiba wa John Mashaka, Dr. H Shayo wa Kule London naye yuko njiani kuelekea Moshi kwenye Kampeni

Je wadau, hii imekaaje? Hawa vijana watatu Mashaka, Shayo,na January ni Chachu mpya au nguvu ya Soda tu? Kama kweli watajitosa ulingoni, basi sura ya Tanzania itabadilika, kwa sababu uwezo wa kubadilisha nchi wanayo na ni majasiri kupambana na ufisadi, na nina uhakika Rais 2015 atakuwa mmoja wa hawa vijana watatu kama siyo Membe

Bila kusahau, ndugu yetu mwanakijiji vipi yeye anagombea wapi?
Tutawapa taarifa zaidi pale tutakapozipata…………………! Endeleeni kukaa mkao wa kula

Mkuu siku nyingine lete habari bila kuweka conclusion zako na ideas zako. Hapa naona tayari wewe ni sehmeu ya kampeni kwa hiyo unajaribu kutuvuta kwa hao jamaa zako.
 
Bahati nzuri kwa Dar yalipo makazi yangu ni Kipunguni-kitunda,na sijaona hata siku moja John Mashaka akishirikiana na sisi kweye suala la maendeleo;kwa ufupi kama kweli anakuja kugombea Ukonga na aje na "tutamnyoa" na hizo" hela zake!Kama suala ni mgombea kiana wapo wengi tu Ukonga na sio lzm awe John Mashaka ambaye umaarufu wake kwa wana Ukonga tunausikia tu kupitia blog ya Michuzi inayomtangaza kweli kweli!

Pia kama kweli ataleta Wamarekani kuja kumfanyia kampeni hapo atakuwa anavunja katiba,sheria mama za uchaguzi wa TZ zinakataza kabisa kwa mtu asiye raia wa tz kuhusika kwa lolote lile ktk uchaguzi wetu kama sisi ambavyo hatuingilii chaguzi za nchi zingine!

"Mwisho ni hii habari ya dola 350,000 na gari hizi zake za kifahari",Kwa maisha ya USA kujikusanya hadi kufikisha hela hizo na kununua magari hayo ni ngumu;anyway acha niamini kama anavyo vitu hivyo,lkn je vitamsadia kupata Ubunge wa Ukonga bila mtaji wa watu?
 
Bahati nzuri kwa Dar yalipo makazi yangu ni Kipunguni-kitunda,na sijaona hata siku moja John Mashaka akishirikiana na sisi kweye suala la maendeleo;kwa ufupi kama kweli anakuja kugombea Ukonga na aje na "tutamnyoa" na hizo" hela zake!Kama suala ni mgombea kiana wapo wengi tu Ukonga na sio lzm awe John Mashaka ambaye umaarufu wake kwa wana Ukonga tunausikia tu kupitia blog ya Michuzi inayomtangaza kweli kweli!

Pia kama kweli ataleta Wamarekani kuja kumfanyia kampeni hapo atakuwa anavunja katiba,sheria mama za uchaguzi wa TZ zinakataza kabisa kwa mtu asiye raia wa tz kuhusika kwa lolote lile ktk uchaguzi wetu kama sisi ambavyo hatuingilii chaguzi za nchi zingine!

"Mwisho ni hii habari ya dola 350,000 na gari hizi zake za kifahari",Kwa maisha ya USA kujikusanya hadi kufikisha hela hizo na kununua magari hayo ni ngumu;anyway acha niamini kama anavyo vitu hivyo,lkn je vitamsadia kupata Ubunge wa Ukonga bila mtaji wa watu?

- Mkuu Malafyale heshima mbele sana mkuu, kumbe mkuu na wewe ni jirani unajua mimi mkuu nipo chini yako hapo Kinyerezi mkuu ukivuka reli tu njia ya kwenda Segerea, saafi sana sasa lazima tuhamishie hii elimu tunayoipata hapa JF mpaka huku jimboni kwetu saafi sana na tupo pamoja.

- Kwa leo sina comments na hizi habari za Mashaka, lakini in due time nitasema, kwanza ni jimbo langu anyways, ngoja niwasiliane na wazee wa jimbo kwanza and then nitasema tena loud and very clear, when the time is right.

Respect.

FMEs!
 
Kama kweli anataka ku-invest hizo dola laki 3.5 lazima aseme kwanza atazirudisha vipi. Hatuwezi tukawa tunafanya kazi ya kuwapigia kelele wezi na kuwakaribisha majambazi, au tukubali kununuliwa na majambazi.
Katika hali ya kawaida mtu mwenye dola laki 3 na 4x4 nne hata jiingiza kwenye "mchezo mchafu", aanze kwanza kwa ku-invest hizo dola kwenye jimbo hilo then tuone kama anawasaidia wananchi, otherwise ni kwamba anataka kuwanunua wananchi ili ajichotee
 
- Mkuu Malafyale heshima mbele sana mkuu, kumbe mkuu na wewe ni jirani unajua mimi mkuu nipo chini yako hapo Kinyerezi mkuu ukivuka reli tu njia ya kwenda Segerea, saafi sana sasa lazima tuhamishie hii elimu tunayoipata hapa JF mpaka huku jimboni kwetu saafi sana na tupo pamoja.

- Kwa leo sina comments na hizi habari za Mashaka, lakini in due time nitasema, kwanza ni jimbo langu anyways, ngoja niwasiliane na wazee wa jimbo kwanza and then nitasema tena loud and very clear, when the time is right.

Respect.

FMEs!

FMEs,Mkandara

Hii tabia kuwa ukiwa na hela basi unaweza kufanya lolote kwenye siasa za TZ lzm zikomeshwe na mwanzo wa ukomeshwaji huo utaanzia kwetu Ukonga!

Kwa leo sina mengi,nikitoka Kyela nitapitiliza kuongea na wazee na vijana pale Kwa njenje,kisha nizunguke kote hadi Kipawa;nisikie wazee na vijana wanasema nini!

FMEs na Mkandara kwa hili tuweke kando tofauti zetu,tunaweza kugswana kata za kuelemisha wapiga kura madhara ya kuifanya Ukonga kama jimbo la "majaribio"yaliyomkuta Mzee Rupia nahisi yatamkuta huyu kijana John Mashaka kwenye sanduku la kura!

Kuandika kizungu kwenye blog ya Michuzi ndiyo tiketi ya kuupata ubunge wa Ukonga?FMEs na Mkandara kwa vile mpo Dar watafuteni wadau kama akina Jerry Slaa kuwauliza wana maoni gani kwa hii issue!
 
Nilishatamka muda si muda mrefu uliopita humu ndani kuwa dude atakuwa ana lake jambo kutokana na historia na juhudi yake ndefu na kubwa ya kujibeza na kutafuta exposure ya dezo kwenye MICHUZI BLOG na hata mainstream media kama Daily News. Naona sasa pay-back time imekaribia, na kama Wamarekani wanavyosema, hamna msosi wa bure! Kaaz kwer kwer!
 
Haka kamjamaa ka-Mashaka kanachekesha kweli..nways time will tell/
 
Kuna habari nyingine huwa naona uchuro kuweka komenti zangu
 
If Mr. Mashaka really has enough money, I advice him to think of investing it somewhere else but not in politics. If he already has an investment, then he would rather think of expanding his current investment or in a completely different venture but not in politics. My professional competence and experience as a political analyst tell me that he has chosen a wrong place to invest his money. I am confident that Mr. Mashaka will loose horribly. To me and perhaps few of you, the reasons are rather obvious.
 
Kama kweli John Mashaka anatumia pesa kwenye kampeni hiyo basi he has spoilt himself and has been rejected outright. In the first place kamnunua michuzi kule kwenye blog yake. Huku nako wewe bwana umeshavuta chako. Vijana gani wazuri wanaengage into dirty politics? Watanzania tuwe waangalifu sana na hao wanaotaka kutumia vijisenti kuingia ktk madaraka. It implies kwamba wakishapata hizo nafasi watataka kurudisha pesa zao. If they have money and skill why don't they venture into business right away? They are just fishy! But I'm happy the community is slowly getting to know how to deal with such things. They won't and shouldn't agree to be bought/fooled!
 
Back
Top Bottom