Joka mwenye vichwa saba


Ngoja nikupigie makofi !!!!!!! Kwa kwa kwa kwaaaa hongeraaaaa, Kwa kwa kwa kwaaaa Imaraaaa, Kwa kwa kwa kwaaaa waaaa
 
Kwanini unahangaika ilhali siku hizi wanajitangaza bila kificho wataalam wa kuwababua? nunua gazeti la Kiu wamejaza kurasa mbili matangazo yao.
 

Wewe umesimuliwa na Kaka yako, mimi nimesimuliwa na Mama yangu mzazi ambae maishani mwake amekulia Matombo ktk maisha yake yote. Yeye ameniambia Nyoka huyu huwa anapita kipindi ambacho kuna mvua kali sana, na mvua hiyo kubwa inaponyesha huyo Nyoka anatoka hapo alipo kwenda Baharini. Ila ameniambia siku hizi haya mambo hayatokei sana, tena alinitajia mpaka jina la huyo nyoka ila nimelisahau.
 
Ngoja nikupigie makofi !!!!!!! Kwa kwa kwa kwaaaa hongeraaaaa, Kwa kwa kwa kwaaaa Imaraaaa, Kwa kwa kwa kwaaaa waaaa

Keshatuambia, hadithi yake alifundishawa na kaka yake, mbona umesahau kumuuliza, hadithi yake inatufundisha nini?
 
Ngoja nikupigie makofi !!!!!!! Kwa kwa kwa kwaaaa hongeraaaaa, Kwa kwa kwa kwaaaa Imaraaaa, Kwa kwa kwa kwaaaa waaaa

afu nyie jamani munafanya matani uku mwenzenu nipo siriaz!basi siwaambii hadisi aliyoniambia babu basi!nyie si munajifanya machi no!basi siwaambii basi!siwambii babu alisema kaona mamba mkubwa baharini siwaambii ng'o,haoo!wamenuna!
 
Watu humu JF sijui wakoje,anyway ni ngumu sana kumuelewesha mjinga,mi niliwahi kufukuzwa na nyoka mwenye vichwa viwili na rangi ya maua,wakati nawinda kware porini nikiwa na umri wa miaka 16 nikiwa na rafiki yangu,hiyo ilikuwa mwaka 2000,karibuni mtengeneze thread ya kukataa,maana huwa hamkubali hadi yawakute.
 

Hahaha, mimi bibi yangu alinisimulia kuwa ziwa victoria lilifanyika siku moja, ardhi ilipasuka na kutitia, viola kitu kikawa ziwa, tena ukimbishia mnagombana, yeye anasema ni kweli tena kuna watu wengi sana walizama pale!..Watu wa zamani kwa saundi! Ukiwa kichwa mbovu na wewe utaamini kama huyu jamaa HARVESTER walivomshika kichwa kisa ni wazazi wake!
 
Last edited by a moderator:

Weee mutoto acha ulongo wako.......!!!!!! mwaka 2000 mapori yalikuwa tayari yamekwisha....... ungesema mwaka 1984 au 1990 ningekubali...... ulivyokuwa ukiviona ni vichaka tu....

 
kweli,hata me nilisikia kwa kuhadithiwa...na anaitwa Nondo...na kwa mujibu nilivyoambiwa ye huwa anaishi chini yaani ndani ya milima/vichuguu na akimove ndo hisababisha earthquake ktk maeneo hayo!..ila hili la utajiri nalickia kwako!!

"Nondo mla watu" nakumbuka huyu alikufa tukiwa darasa la tatu, maana alimeza watu wengi lakini kuna dogo alimezwa akiwa ana kisu akalichoma lile joka watu wakatoka maana joka lilikufa hapo hapo.

Kwa hiyo Nondo alishakufa.

Tukirudi kwenye hii stori, mi najua tetemeko la ardhi linatokana na joka kubwa duniani lililoko chini ya ardhi linapokuwa linageuka.
 

sasa ndg kumbe unahadhina tele ya taarifa kuhusu hilo joka.mbona unatuuliza cc tena.!!
 

hilo joka lina magamba ambayo kitaalamu tunayaita "tectonic plates",na likigeuka linatema uji wa moto kitaalamu tunauita "magma" teh teh!
 
Sijajua how serious this discussion is,manake great thinkers wana njia zao nyingi za kuelimishana na ukiingia kichwa kichwa unaweza ukadhani ni upuuzi unaendelea kumbe "mzigo" ndio unatafunwa taratibu.Nijiunge kutafuna haka kamzigo,ngoja nitafute pa kung'ata,wakuu mie siamini kama majini na mashetani yapo kweli!nyie mnasemaje?
 
hilo joka lina magamba ambayo kitaalamu tunayaita "tectonic plates",na likigeuka linatema uji wa moto kitaalamu tunauita "magma" teh teh!

Umechanganya kaka, tectonic plates ni kuta zinazolifunika hilo joka, ambapo likijigeuza ndio hizo kuta zinatikisika na kusababisha tetemeko la ardhi. Kwenye magma hata mi sijapajua, sidhani kama panatokana na joka kuu.
 
Huyo mnaosemea joka mwenye vichwa saba hata mimi nilisikia it might be ni myth

ila ile ya kwenye biblia kwenye ufunuo joka mwenye vichwa saba
ni ofcourse ni G7
 
Umechanganya kaka, tectonic plates ni kuta zinazolifunika hilo joka, ambapo likijigeuza ndio hizo kuta zinatikisika na kusababisha tetemeko la ardhi. Kwenye magma hata mi sijapajua, sidhani kama panatokana na joka kuu.

mkuu naona unatupeleka kwenye hindu mythology sasa.Kwamba mungu ni roho inayoishi ndani ya viumbe wote wenye asili yake(divine beings),the so called brahman.Kwamba aliumba gods and anti-gods ili kuleta usawa katika spiritual realm kati ya wema na ubaya(metaphysics hii).Kwamba kule kwa miungu kuna wakuu watatu ambao ni Brahma(aliyetumika kuumba dunia na viumbe wote),Vishnu(anayeilinda na kuiendeleza dunia na viumbe wote),na Sheva(atakayekuja kuangamiza dunia ili iumbwe tena).Kwamba kule kwa antigods(wapinzani wa miungu na wema)kuna race ya miungu-viumbe(demigods)inayoitwa Naga ambao ni majoka.Kwamba mfalme wa Nagas aliyeitwa Shesha hakupendezwa na kutenda uovu kama wenzie akaamua kujitenga na kufunga,kumeditate na kujitesa hadi mungu Brahma akamuonea huruma na kumuambia aombe chochote.Shesha akatoa ombi lake lililomfanya apewe kazi ya kukaa chini ya dunia na kusimamia sayari zote zisiyumbe.Akawa mhimili wa dunia.Kwamba huyo Shesha akijikunjua,dunia inaumbwa,akijikunja dunia inafika mwisho,akijigeuza dunia inatetemeka na ndipo mafuriko na matetemeko yanatokea.Kazi ipo jamani na dini zetu hizi!huenda hii ni connection na myths za nondo mla watu?manake zote ni ancient stories.But i'm becoming suspicious here,kwa nini hadithi za majoka?wachina dragons,wahindi serpents,latinos reptilians,wazungu shape shifters,waafrika nondo mla watu,hata bible ina kitu kinaitwa "kizazi cha nyoka"!kuna nini hapo?well,lisemwalo lipo na kama halipo.....
 

Unajua mfumo mzima wa Dunia kuzunguka jua, kupatwa kwa mwezi na jua, matetemeko, ile tumeambiwa Continental Drifts, mambo ya volcano na mengine ya sisi kuwa juu ya dunia inayozunguka wakati sisi tumetulia wana sayansi hawayaelezei haya mambo kwa ufafanuzi yakinifu, wanabaki kutuambia ni "Nature", baada ya kutoelezea vizuri ndio wengine wanakuja na mawazo yao ya nini chanzo, hapa zinaibuka hizo myth za majoka, ambazo ukireason kama layman unaona zina logic kupita maelezo ya wana sayansi.

Mfano, nikiwa mdogo niliambiwa mvua inatokana na mvuke, kwamba jua linapowaka linayeyusha maji ya chini yanapanda juu na kuganda, yanapoyeyuka ndo mvua inanyesha; katika kuvalidatate hii statement nikaambiwa eti ndio maana jua likiwaka sana watu wanasema leo mvua itanyesha na inanyesha; nikauliza mbona kiangazi mvua hainyeshi wakati ndio jua linawaka sana? Nikaambiwa mavingi ni makavu.

Siku moja akatokea mtu akatuambia kule Mbinguni (angani) Mungu ana mapipa mengi sana amejaza maji, sasa akitaka mvua inyeshe anaangusha mapipa yale upande unaohusika na mvua inanyesha, akasema zile radi tunazozisikia ni mgongano wa hayo mapipa yanapokuwa yanagalagala. Na pia jamaa akasema ndio maana mvua inaweza kunyesha hapa kwetu lakini kwingine isinyeshe, ni kwa sababu mapipa yameangukia upande wetu. Sasa kama hapa utamwelewa nani?
 
jamani naipenda jamii forum kama hv ningecheka saa ngapi? kwani we hujamuona na yule samaki nusu mtu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…