eliakeem
JF-Expert Member
- May 29, 2009
- 17,214
- 15,853
Mbona mnamuharibia uzi wake jamani?mwenzenu yuko serious nyie mnaanzisha "zero brain"!jf bhana!kaka yangu aliwahi kukutana na story hizo zamani milima ya uluguru.Alikwenda kumsalimia babu.Siku moja akiwa huko kijijini pale walifanya matambiko halafu kesho yake mvua na upepo mkali ikaanza kunyesha.Wazee wakaamuru watu wote waingie ndani.Mvua ilipoisha babu akamshika mkono hadi nje eneo lenye mashamba na kukuta kila mtu yuko huko.Kulikuwa na barabara kuubwa imetengenezwa porini,imejaa magamba makubwa sana chini.Babu akamwambia kaka kuwa huyo ni joka wa mizimu.Huwa anapaa na kwenda baharini kila baada ya miaka fulani.na watu wa pale wanaelewa habari yake vizuri tu.Sasa sijui kaka nae alinidanganya?binafsi nilikutana na mambo ya ajabu ajabu Matombo,kijiji cha Mvuha,kule Moro hadi leo siyaelewi ila tukisema hapa tunaonekana wachawi!ila ilikuwa rahisi kwenu kuamini lile joka la Misri?.au kwa vile mliona picha?Hayo maviumbe yapo sema mara nyingi huwa na mauzauza!waulizeni wafanyabiashara wa mazao ya misitu kama mbao,kuna misitu hawaingii kukata miti hadi wafanyiwe matambiko na wenyeji,kuna mambo ya ajabu sana duniani hapa sijui kwa nini hayasemwi na media.
Ngoja nikupigie makofi !!!!!!! Kwa kwa kwa kwaaaa hongeraaaaa, Kwa kwa kwa kwaaaa Imaraaaa, Kwa kwa kwa kwaaaa waaaa