Jokate: Ali Kiba ndiyo nani???

Jokate: Ali Kiba ndiyo nani???

figganigga

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
25,724
Reaction score
55,906
Dar es Salaam: Mwanamitindo Jokate Mwegelo amegeuka ‘Mbogo’ baada ya kuulizwa habari inayohusiana mwanamuziki Ali Kiba.
DjCQBNzWsAAS2J2.jpg

Jokate Julai 26.2018 alitia timu katika arobaini ya mtoto wa mtangazaji Zamaradi Mketema ilipofanyika nyumbani kwake Bunju, jijini Dar es Salaam.

Alipoingia tu, watu waliohudhuria katika arobaini hiyo waligeuka kumuangalia kama wamepatwa na mshangao huenda kwa kitendo chake cha kupotea kwa kipindi kirefu machoni mwa watu.

MCL Digital ilimtafa alipokaa na kuzungumza naye mambo machache juu ya ukimya wake, ilianza na swali la kutoonekana mitandaoni tu baada ya Mwanamuziki Ali Kiba kufunga ndoa.

"Noooo sitaki utaje jina la Ali Kiba, ukitaka tuzungumze uliza kitu bila kuweka hilo jina na nikwambie tu mimi sijakimbia mitandaoni nipo sana, sema watu wanashindwa kuniona sababu mara nyingi nakuwa nacomment kwenye kurusa za watu haswaa nikiona kitu kimenivutia

"Kitu kingine ni ubize na majukumu yangu, ndio yanayoniweka kimya kwenye masuala mengine," alisema Jokate

Jokate ambaye kimuonekano ukimuangalia amenenepa na kuzidi kunawili, ila ule ujauzito aliokuwa anadaiwa anao, hakuna hata dalili ya kuonekana.

MCL Digital iliendelea kumuuliza habari za madai ya kuwa na ujauzito, Jokate mitandaoni kuna mambo mengi acha na hilo swali.

"Hayo mambo ya mitandaoni ungeyaacha tu, hilo swali hapana kwangu"

Aidha Jokate amesena kila kinachoongelewa mitandaoni anavisoma na kuvipotezea kwani amegundua wapo watu hawajui matumuzi ya mitandao wanatakiwa wapate elimu.
 
Ila huyo mwandishi nae mmbea. Kuuliza swali la mtego ili iweje wakati mwenzie kakaa pazuri sasa hivi. Jokate kazuri sana nako
Samahani dada, mi mgeni humu!! Jokate kakaa pazuri sasa hivi?! Kivipi yaani?! Ni kwamba kahamia mtaa mzuri au amehamia nyumba mzuri?

Halafu kuna mtu nipo jirani nae hapa; ye ndo ananichanganya zaidi! Huyu ameanza kwa kusema issue sio Kiba bhana, kisha akahoji "...yaani sheria ya mitandao aikomalie kwingine halafu unatarajia aache maslahi yake yarande rande mitandaoni!"

Kila nikiuliza, nani huyo unayesema sheria ya mitandao aikomalie kwingine, jamaa anakausha!!! What's going on?!
 
Anakaa posta siku hizi mkuu ndo maana nimesema anakaa pazuri. Si unajua Posta hamna makelele kama huku uswahilini kwetu eeh
 
Back
Top Bottom