Cute Wife
JF-Expert Member
- Nov 17, 2023
- 1,906
- 5,000
Wakuu,
Ya kweli hayo?
Kupata nyuzi za kimkoa Uchaguzi Serikali za Mitaa ingia hapa: LGE2024 - Special Thread: Orodha ya Mijadala ya Mikoa yote Tanzania Bara inayoshiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
=====
Katibu Mkuu wa UVCCM, Jokate Mwegelo, amezindua rasmi kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika Mkoa wa Pwani leo November 20,2024 ambapo pamoja na mambo mengine amesema CCM haijauchukulia poa uchaguzi huo wala kuuona ni mdogo na wa kawaida bali imeuchukulia kwa uzito ndio maana imeshambulia Mikoa yote 26 kwa kuweka Wagombea na kupeleka vikosi vizito vya Viongozi kuomba kura.
Akiongea na Wananchi, KM Jokate amesema “CCM tumezindua rasmi kampeni kwa kupeleka vikosi vizito ili kuwaonesha Wananchi kwamba CCM ndio Chama kinachoheshimu demokrasia, hatujauchukulia huu uchaguzi kama mdogo au wa kawaida, tumeuchukulia kwa uzito wake ndio maana tumeshambulia Mikoa yote”
“Mpaka sasa ili kuonesha jinsi CCM ilivyodhamiria kwamba huu uchaguzi unatuhusu, tumeonesha tupo serious na uchaguzi kuliko Vyama vingine sisi tumeweka Wawaklishi Vijiji vyote na Vitongoji kwa 100%, wenzetu wa upinzani wameshindwa kujaza Vijiji vyote, mpaka sasa kwa jinsi tulivyojitokeza kushiriki uchaguzi huu tumeshashinda uchaguzi huu kwa 64% , leo tunaanza safari ya kutafuta asilimia zilizobaki, niwaombe Wananchi CCM dhamira yake imekuwa sio tu kushika Dola bali kuwahudumia Wananchi, hivyo tunaomba Wananchi mtupe kura CCM”
Soma: Pwani: Matukio yanayojiri kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Novemba 27, 2024