Jokate Mwegelo Aainisha Mapinduzi Makubwa Katika Sekta ya Elimu Zanzibar

Jokate Mwegelo Aainisha Mapinduzi Makubwa Katika Sekta ya Elimu Zanzibar

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

📌📌KOMREDI JOKATE MWEGELO (MNEC) AAINISHA MAPINDUZI MAKUBWA KATIKA SEKTA YA ELIMU ZANZIBAR

Asema Vijana wanayo kila Sababu ya Kumuunga Mkono Dkt. Mwinyi

Mambo Mengi makubwa Dkt. Mwinyi ameyafanya kwa Kipindi Kifupi

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Konresi Jokate Urban Mwegelo (MNEC) ameainisha Mapinduzi Makubwa ya Elimu yaliyofanyika ndani ya Serikali ya Awamu ya 8 inayoongozwa na Mhe Dkt Hussein Ali Mwinyi Zanzibar.

"Pamoja na kwamba kuna hatua kubwa za kimaendeleo zilizofikiwa Zanzibar tangu Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar hadi sasa, kipekee yapo mambo mengi makubwa yaliyofanyika ndani ya kipindi hiki cha miaka mitatu ya Serikali ya Awamu ya Nane, inayoongozwa na Dkt. Hussein Mwinyi, Makamu Mwenyekiti wa CCM, Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi."

"Ndugu Vijana wenzangu Serikali ya Dkt Mwinyi imeweza kuwapatia jumla ya vijana 22,547 (Wanaume 11,485 na Wanawake 11,062) mafunzo ya Amali, Elimu ya Ufundi, Kazi za Mikono, ujasiriamali na Sanaa. Pamoja na hayo, Serikali imefanikiwa katika mambo yafuatayo makubwa yafuatayo"


1. Ujenzi wa shule za awali msingi na sekondari

2. Ujenzi wa vyuo vya kati na vyuo vikuu

3. Uwekaji wa vifaa vya kusomea shuleni na vyuoni

4. Ajira za walimu na upandishaji wa mishahara ya walimu

5. Utoaji wa mikopo ya elimu ya juu kwa vijana wakizanzibari waliokosa mikopo ya Jamuhuri ya Muungano wa tanzania.

Aidha Komredi Jokate Mwegelo hayo ni machache miongoni mwa Mambo mengi ambayo yanawagusa Vijana Moja kwa Moja yaliyofanywa na Dkt Mwinyi, hivyo Vijana wanayo kila sababu ya kummunga Mkono kwa kazi zake kubwa alizowafanyia kwa kipindi kifupi.

#KulindaNaKujengaUjamaa
#SisiNaMamaMleziWaWana
#Kaziiendelee

Imetolewa na;
Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi UVCCM Taifa.
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2024-04-20 at 16.49.03.jpeg
    WhatsApp Image 2024-04-20 at 16.49.03.jpeg
    286.6 KB · Views: 7
  • WhatsApp Image 2024-04-20 at 16.49.04.jpeg
    WhatsApp Image 2024-04-20 at 16.49.04.jpeg
    155 KB · Views: 6
  • WhatsApp Image 2024-04-20 at 16.49.07(1).jpeg
    WhatsApp Image 2024-04-20 at 16.49.07(1).jpeg
    315.2 KB · Views: 8
  • WhatsApp Image 2024-04-20 at 16.49.08.jpeg
    WhatsApp Image 2024-04-20 at 16.49.08.jpeg
    310.3 KB · Views: 6
  • WhatsApp Image 2024-04-20 at 16.49.10.jpeg
    WhatsApp Image 2024-04-20 at 16.49.10.jpeg
    322.2 KB · Views: 6
  • WhatsApp Image 2024-04-20 at 16.49.11.jpeg
    WhatsApp Image 2024-04-20 at 16.49.11.jpeg
    248.3 KB · Views: 6
Ana taaluma gani ya elimu hadi yeye ndo awe wa kwanza kuainisha masuala ya elimu tena nchi ya watu?! Uchawa ni mzigo sana😡😡. Kwamba atoke Bara aende Zanzibar kuainisha masuala ambayo si ya Muungsno huko? Msiwatanie wazanzibari.
 
Komeedi Jokate ebu ondoa huu ujinga hapa. Mtu usiekuwa na elimu unaainishaje mapinduzi katika elimu!!
 
Back
Top Bottom