Jokate Mwegelo apewa tuzo ya ubalozi wa Afya ya Akili

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2013
Posts
790
Reaction score
964
CDE JOKATE APEWA TUZO YA UBALOZI WA AFYA YA AKILI

31 MEI, 2024
UVCCM HQ

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) - Cde. Jokate Urban Mwegelo apewa Ubalozi wa afya ya akili kutoka Hospitali ya Taifa ya Afya ya akili Mirembe leo Mei 31,2024 jijini Dodoma ambapo majukumu yake yatakuwa kusaidia kutoa elimu ya ufahamu kuhusu Afya ya akili hususani kwa Vijana.

Ubalozi huo amepata kufuatia mwaliko aliopewa na Mkurugenzi wa hospitali hiyo ambapo pamoja na mambo mengine amepata elimu kuhusu afya ya akili na Changamoto ya akili kwa namna inavyowakabili Watumishi wanaofanya kazi kwenye ofisi mbalimbali, Wapambanaji wengine kwenye majukumu yao ya utafutaji, Vijana na Wanawake baada ya kujifungua.

Imetolewa na
Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi UVCCM-Taifa.

IMG-20240601-WA0002(1).jpg
 
Mwanya,macho makubwa,matege,wowowo lililozidi nk ni abnormalities. Vipi kuhusu kidoti?Usijibu.
Najibu.Kidoti kile kinatoka kwa mungu watu wengi huzaliwa nacho na hata Mimi (nguva jike) ninacho hicho kidoti.Watu wenye vidoti hivyo sio wa kawaida ni watu wenye......
 
Matege,mwanya,wowowo kubwa(siyo la Uturuki wala kwa dkt Mloganzila),macho makubwa vinatoka wapi?
 
Joketi aliwahi kuwa DC ana kidoti cheusi juu usoni kinapendeza kwelikweli.
Alikuwa DC Kisarawe kabla ya Temeke na Korogwe.

Huku ameacha alama ikiwemo kukuza utalii, kubuni vyanzo vya mapato.

Pia kuna Shule ya Sekondari yenye jina lake huku Kisarawe ambayo ilijengwa kwa ushawishi wake.

Joketi ana kipaji na aliwafaa sana pale UWT lakini sijui ilikuwaje akashushwa!
 
Huko alipopewa ubalozi ndo panamfaa
 
CDE JOKATE APEWA TUZO YA UBALOZI WA AFYA YA AKILI

31 MEI, 2024
UVCCM HQ

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) - Cde. Jokate Urban Mwegelo apewa Ubalozi wa afya ya akili kutoka Hospitali ya Taifa ya Afya ya akili Mirembe leo Mei 31,2024 jijini Dodoma ambapo majukumu yake yatakuwa kusaidia kutoa elimu ya ufahamu kuhusu Afya ya akili hususani kwa Vijana.

Ubalozi huo amepata kufuatia mwaliko aliopewa na Mkurugenzi wa hospitali hiyo ambapo pamoja na mambo mengine amepata elimu kuhusu afya ya akili na Changamoto ya akili kwa namna inavyowakabili Watumishi wanaofanya kazi kwenye ofisi mbalimbali, Wapambanaji wengine kwenye majukumu yao ya utafutaji, Vijana na Wanawake baada ya kujifungua.

Imetolewa na
Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi UVCCM-Taifa.

View attachment 3005473
CDE ndio nini??
 
Back
Top Bottom