Jokate Mwegelo apewa tuzo ya ubalozi wa Afya ya Akili

Jokate Mwegelo apewa tuzo ya ubalozi wa Afya ya Akili

CDE JOKATE APEWA TUZO YA UBALOZI WA AFYA YA AKILI

31 MEI, 2024
UVCCM HQ

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) - Cde. Jokate Urban Mwegelo apewa Ubalozi wa afya ya akili kutoka Hospitali ya Taifa ya Afya ya akili Mirembe leo Mei 31,2024 jijini Dodoma ambapo majukumu yake yatakuwa kusaidia kutoa elimu ya ufahamu kuhusu Afya ya akili hususani kwa Vijana.

Ubalozi huo amepata kufuatia mwaliko aliopewa na Mkurugenzi wa hospitali hiyo ambapo pamoja na mambo mengine amepata elimu kuhusu afya ya akili na Changamoto ya akili kwa namna inavyowakabili Watumishi wanaofanya kazi kwenye ofisi mbalimbali, Wapambanaji wengine kwenye majukumu yao ya utafutaji, Vijana na Wanawake baada ya kujifungua.

Imetolewa na
Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi UVCCM-Taifa.

View attachment 3005473
Mgonjwa sugu wa afya ya akili amepewa tuzo ya kuwa balozi wa Afya ya Akili au sababu ni tofauti na hiyo?
 
Back
Top Bottom