GE2025 Jokate: Vijana CCM baada ya Uchaguzi Makundi yavunjike, turudi Mezani kuijenga Jumuiya Yetu, na Chama

GE2025 Jokate: Vijana CCM baada ya Uchaguzi Makundi yavunjike, turudi Mezani kuijenga Jumuiya Yetu, na Chama

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Jokate Mwegelo, amesema vijana wanapaswa kuendeleza misingi ya ujamaa, amani, upendo na mshikamano hata baada ya kukamilika kwa uchaguzi wa wabunge wa viti maalumu ndani ya jumuiya hiyo.

Ametoa wito kwa vijana wa CCM kutambua kuwa siasa siyo uadui, bali ni mchakato wa kujenga na kuimarisha chama.

Amesema chama kimejengwa juu ya misingi imara ya kiuongozi inayolenga kuleta maendeleo kwa wote, hivyo ni muhimu kwa vijana kuacha makundi mara tu baada ya kupatikana kwa washindi, na badala yake kurudi pamoja kuijenga jumuiya kwa umoja na mshikamano.

Amesisitiza kuwa mshikamano wa vijana ni msingi wa ushindi wa CCM katika uchaguzi wowote ule.

Jokate amewahimiza vijana kujitokeza kwa wingi kupiga kura kwa umakini, kwa kuzingatia sifa, uwezo na uadilifu wa wagombea.

Amesema ni muhimu kuchagua viongozi watakaoweza kubeba ajenda za vijana na kuwawakilisha kwa ufanisi ndani ya chama na serikali kwa ujumla.

Aidha, amewataka vijana kutumia haki yao ya kupiga kura kwa weledi na utimamu wa akili, wakitambua kuwa maamuzi yao yatakuwa na athari ya moja kwa moja kwa maendeleo ya kizazi cha sasa na kijacho. Jokate amesema UVCCM itaendelea kuimarisha misingi ya uongozi bora na kuwa chachu ya mabadiliko chanya katika jamii.

 
Umenikumbusha mbali kipindi wote tunatafuta namna ya Kuwatumikia Watanzania katika njia za Uwajibikaji na Haki hakika ulifanikisha Projects nyingi za Vijana kwa Wakati huo,na Hii kauli ilikuwa Msemo Baada ya Chaguzi za Vyuo Ameen🇹🇿🇹🇿🇹🇿🙏
 
Back
Top Bottom