Jomo Kenyatta (56) na Abdul Sykes (26) Katika Mkutano wa Siri, Nairobi 1950

Jomo Kenyatta (56) na Abdul Sykes (26) Katika Mkutano wa Siri, Nairobi 1950

MZEE HONGERA kwa kuweza bakiza historia ambayo kizazi chetu na wazee wetu wamekua wavivu kuandika labda makusudi au kutokutaka..nikitaka nakala ya hiki kitabu naweza kukipataje?
Numbisa,
NIngeandika kitabu changu kwa nia ya kumdogosha Mwalimu Nyerere kitabu kingekufa na sidhani kama ningeweza kupata mchapaji wa maana na vilevile kuweza kupata mialiko kutoka kwa wasomi wa historia ya Afrika.

Halikadhalika kitabu kisingependwa kwa kufikia kuchapwa sasa mara nne na tunakwenda toleo la tano.

Mimi napongezwa kote hakuna anaenihurumia.
Hivi sasa nishapokea nishani tano kwa kazi hii.

Mimi nakupa pole wewe.

View attachment 2990908
 
MZEE HONGERA kwa kuweza bakiza historia ambayo kizazi chetu na wazee wetu wamekua wavivu kuandika labda makusudi au kutokutaka..nikitaka nakala ya hiki kitabu naweza kukipataje?
Cmon...
Kitabu kinauzwa Ibn Hazm Media Centre kwenye maduka yao yapo Msikiti wa Mtoro, Manyema, Mtambani na Kichangani bei 10 000.00.

Kipo kwa Kiingereza na Kiswahili.
 
Nakuona mdini
Vichekesho,
Mimi nakuona huna uwezo wala ujasiri kwa kukubali ukweli.

Wataalamu wa African History: John Iliffe, Jonathon Glassman na James Brennan wao baada ya kusoma kitabu wakafanya review zao na zikachapwa katika Cambridge Journal of African History.

Jonathon Glassman akanialika chuoni kwake Northwestern University, Evanston, Chicago nikazungumze.

Naamini unajua uzito wa jambo hili.

Amesha silimu?
 
Mzee hicho kilichoandikwa na Abdul Sykes kama historia ya TANU siyo rasmi na itasalia kuwa daraja kwa waaminio
Uzalendo...
Kitabu kimeandikwa na mimi.
Wasomaji ndiyo wanaoamua hatima ya kitabu.

Kitabu hiki kimependwa sana.

Kimechapwa mara nne kwa Kiingereza na Kiswahili.
 
IKIWA HUJAPATAPO KUZIONA TARIFA ZA KIKACHERO ZA SPECIAL BRANCH 1950s
"Tanganyika Political Intelligence Summary, March 1952":

"...it is reported that the Secretary of the Association, Abdul Wahid Sykes has dispatched letters to all branches asking members for suggestions under the following heads for a memorandum to be prepared for the Royal Commission..."

...Abdul Wahid Kleist Sykes, Secretary of the African Association who, as reported in last month's summary (paragraph 20) was going on safari up country, visited Mwanza, where he met Paul Bomani, President of the Bukoba African Association, and accompanied him to Bukoba. Sykes then visited Kampala alone..."

Mwaka huu wa 1950 Abdul Sykes akiwa Secretary wa TAA na mjumbe wa TAA Political Subcommittee, Abdul alikuwa na umri wa miaka 26.

Kijana mdogo sana.
Jomo Kenyatta alikuwa na miaka 56.

Jomo Kenyatta kazaliwa mwaka wa 1894 sawasawa na umri wa Kleist Sykes baba yake Abdul ambae alikuwa kafariki mwaka wa 1949.

Utaweza vipi kuandika historia ya TANU na harakati za kudai uhuru wa Tanganyika ukaacha historia kama hii na wala usiwataje wahusika wa harakati hizi?

Kisha anatokea mtu anasema kuwa chama cha TAA kilikuwa chama cha starehe.

Ningeweza kueleza mengi katika uandishi wa historia ulifanywa na Chuo Cha CCM Kivukoni lakini tutosheke na haya.

Kila nipitapo mitaa ya Maktaba nakutana na kumbukumbu hizi.

Hizi ni taarifa kutoka Rhodes House Library, Oxford kutoka majalada ya kikachero ya Waingereza baada ya miaka 50 yanawekwa wazi kwa mtafiti yeyote kuyasoma na kufanya nakala akipenda.

Historia hii alinihadithia Mzee Ahmed Rashaad Ali tumekaa nyumbani kwake Ali Hassan Mwinyi Road tunazungumza.

Ahmed Rashaad Ali ni huyo kuliwa kwa Jomo Kenyatta.

Mzee Rashaad aliniomba nisimtaje jina katika kitabu cha rafiki yake Abdul Sykes nilichokuwa natafiti.

Wakati huo nilikuwa sijapata nyaraka hii ya Special Branch.

Siku nilipoletewa nyaraka hii nilinyanyua mikono juu kumshukuru Allah kwa kuthibitisha kile ambacho Mzee Rashad alinieleza.

Wakati huu Mzee Rashad alikuwa tayari keshafariki.

Huko tulikotoka miaka hiyo watu walikuwa wakihofu kueleza historia ya kweli ya TANU.

Hakika tumetoka mbali na leo ukweli umedhihiri.

Mohammed Said wewe ni kuongelea udini tu hadi utakufa, kwanini umekuwa brainwashed to that extent? Shauri yako, ulevi wa dini mbaya sana, ni utumwa usio na mwisho
 
Mohammed Said wewe ni kuongelea udini tu hadi utakufa, kwanini umekuwa brainwashed to that extent? Shauri yako, ulevi wa dini mbaya sana, ni utumwa usio na mwisho
Jay...
Mwenye udini si mimi.

Mwenye udini ni wewe unaechukia kusoma historia ya Waislam.

Historia hii inayokuumiza ilifutwa mimi nimeirejesha.

Sasa udini uko wapi.
Wewe ulitakaje?

Kuwa isiwepo?

Historia hii ya Kenyatta na Abdul Sykes wapi imezungumza kuhusu Uislam?

Mimi nimealikwa vyuo vingi na nimezungumza.

Kazi zangu zimechapwa na wachapaji vitabu wa sifa kama Oxford University Press unataka kusema hawa hawakuona udini katika maandishi yangu?
 
JPM si alitoka kwenye ubunge, kaingia uwaziri utendaji wake ukaonekana.

Huyu rais wa sasa si inajulikana ni kwa mujibu wa katiba.

Nyerere ilikuaje ametoka Butiama na bukta kuchunga ng'ombe na kulima aje kuwazidi visiki wa mjini wenye mji wao? Ni swali najiuliza tu, kwa sababu hadi leo wajukuu na watoto wa wazee wale wa mjini hawaachi kulalama nao wanashangaa ilikuaje mzanaki yule akawazidi akili wazee wao?

Kwa upande mmoja mchonga aliwazidi akili wale wazee, akageuza mchezo mzima juu chini na chini juu, kimekua kilio kuanzia wazee hadi wajukuu.
Elimu elimu.
 
Elimu elimu.
Covid...
Soma kwanza historia ya Nyerere ndiyo umzungumze.

Katika kitabu cha maisha yake kilichoandikwa na Prof. Shivji, Prof. Saida Othman Yahya na Dr. Ng'wanza Kamata wamesema kuwa katika utafiti wa kuandika maisha ya Mwalimu wamekuta maktaba tatu zenye taarifa nyingi za Mwalimu.

Maktaba ya kwanza ni ya Dr. Salim Ahmed Salim kisha ya Mohamed Said na ya tatu ya Brig. General Hashim Mbita.

Nyerere amekuja Dar-es-Salaam 1952 haada ya kumaliza masomo University of Edinburgh.

Hakuja Dar es Salaam kavaa bukta.

Nyerere kapokelewa na Abdul Sykes umri wake miaka 28.

Nyerere hakupokelewa na wazee.

Kakuta Abdul yuko katika mipango ya kuibadili TAA kuwa chama kamili cha siasa akiwa Secretary na Act. President.

Nyerere kaikuta TAA kupitia TAA Political Subcommittee iko katika mipango ya kwenda UNO.

Nyerere kaingizwa katika uongozi baada ya kupendekezwa na Hamza Mwapachu.

Historia hii nimeieleza hapa mara nyingi.

Nyerere kaingia kwenye chama ambacho kiliasisiwa mwaka wa 1929 na Kleist Sykes (35) baba yake Abdul na vijana wengine wa Dar-es-Salaam kama Mzee bin Sudi (33)na Ibrahim Hamisi kwa kuwataja wachache.

Baadhi ya waasisi hawa Nyerere kawakuta ndani ya TAA Abdul akiwa kiongozi kama Mzee bin Sudi, Ramadhani Mashado Plantan, Schneider Abdillah Plantan na kaka yao Saudtz Thomas Plantan kwa kuwataja wachache.

Historia ya uchaguzi wa mwaka 1953 baina ya Abdul Sykes na Nyerere katika nafasi ya Rais wa TAA nimeieleza mara nyingi.

Sasa hicho alichopindua Nyerere kipi?

Hebu kieleze kifahamike.

Au unakusudia kuuliza imekuwaje Nyerere hakupata kuieleza historia hii muhimu maishani kwake?

Historia hii si ndiyo hii inajadiliwa hapa sasa zaidi ya miaka 10?

Sasa hicho kilichopinduliwa ni kipi?
 
Kuna kitu ambacho kimetengenezwa Tanzania kutohoji chochote kinachogusa..dini..Mimi ni mkatoliki...ila ni muumini wa kupenda ijua historian...kwakua katika vyote....mda ndo jibu na dawa ya kutenganisha ukweli na uongo...Bado naamini kwa kizazi chetu na kijacho...Tunahitaji sana maandiko tujifunze tulipotoka na tunapoelekea...ntakifuata kitabu mzee
 
Cmoney,
Ahsante sana.
 
Cmon...
Kitabu kinauzwa Ibn Hazm Media Centre kwenye maduka yao yapo Msikiti wa Mtoro, Manyema, Mtambani na Kichangani bei 10 000.00.

Kipo kwa Kiingereza na Kiswahili.
sisi wa mikoani,tuomba mawasiliano tuweze kutumiwa
 
Back
Top Bottom