Jomo Kenyatta (56) na Abdul Sykes (26) Katika Mkutano wa Siri, Nairobi 1950

MZEE HONGERA kwa kuweza bakiza historia ambayo kizazi chetu na wazee wetu wamekua wavivu kuandika labda makusudi au kutokutaka..nikitaka nakala ya hiki kitabu naweza kukipataje?
 
MZEE HONGERA kwa kuweza bakiza historia ambayo kizazi chetu na wazee wetu wamekua wavivu kuandika labda makusudi au kutokutaka..nikitaka nakala ya hiki kitabu naweza kukipataje?
Cmon...
Kitabu kinauzwa Ibn Hazm Media Centre kwenye maduka yao yapo Msikiti wa Mtoro, Manyema, Mtambani na Kichangani bei 10 000.00.

Kipo kwa Kiingereza na Kiswahili.
 
Cmon...
Kitabu kinauzwa Ibn Hazm Media Centre kwenye maduka yao yapo Msikiti wa Mtoro, Manyema, Mtambani na Kichangani bei 10 000.00.

Kipo kwa Kiingereza na Kiswahili.
Tupe namba zao tukiagize kwa sisi tulip nje ya DSM.
 
Nakuona mdini
Amesha silimu?
 
Mzee hicho kilichoandikwa na Abdul Sykes kama historia ya TANU siyo rasmi na itasalia kuwa daraja kwa waaminio
Uzalendo...
Kitabu kimeandikwa na mimi.
Wasomaji ndiyo wanaoamua hatima ya kitabu.

Kitabu hiki kimependwa sana.

Kimechapwa mara nne kwa Kiingereza na Kiswahili.
 
Mohammed Said wewe ni kuongelea udini tu hadi utakufa, kwanini umekuwa brainwashed to that extent? Shauri yako, ulevi wa dini mbaya sana, ni utumwa usio na mwisho
 
Mohammed Said wewe ni kuongelea udini tu hadi utakufa, kwanini umekuwa brainwashed to that extent? Shauri yako, ulevi wa dini mbaya sana, ni utumwa usio na mwisho
Jay...
Mwenye udini si mimi.

Mwenye udini ni wewe unaechukia kusoma historia ya Waislam.

Historia hii inayokuumiza ilifutwa mimi nimeirejesha.

Sasa udini uko wapi.
Wewe ulitakaje?

Kuwa isiwepo?

Historia hii ya Kenyatta na Abdul Sykes wapi imezungumza kuhusu Uislam?

Mimi nimealikwa vyuo vingi na nimezungumza.

Kazi zangu zimechapwa na wachapaji vitabu wa sifa kama Oxford University Press unataka kusema hawa hawakuona udini katika maandishi yangu?
 
Elimu elimu.
 
Elimu elimu.
Covid...
Soma kwanza historia ya Nyerere ndiyo umzungumze.

Katika kitabu cha maisha yake kilichoandikwa na Prof. Shivji, Prof. Saida Othman Yahya na Dr. Ng'wanza Kamata wamesema kuwa katika utafiti wa kuandika maisha ya Mwalimu wamekuta maktaba tatu zenye taarifa nyingi za Mwalimu.

Maktaba ya kwanza ni ya Dr. Salim Ahmed Salim kisha ya Mohamed Said na ya tatu ya Brig. General Hashim Mbita.

Nyerere amekuja Dar-es-Salaam 1952 haada ya kumaliza masomo University of Edinburgh.

Hakuja Dar es Salaam kavaa bukta.

Nyerere kapokelewa na Abdul Sykes umri wake miaka 28.

Nyerere hakupokelewa na wazee.

Kakuta Abdul yuko katika mipango ya kuibadili TAA kuwa chama kamili cha siasa akiwa Secretary na Act. President.

Nyerere kaikuta TAA kupitia TAA Political Subcommittee iko katika mipango ya kwenda UNO.

Nyerere kaingizwa katika uongozi baada ya kupendekezwa na Hamza Mwapachu.

Historia hii nimeieleza hapa mara nyingi.

Nyerere kaingia kwenye chama ambacho kiliasisiwa mwaka wa 1929 na Kleist Sykes (35) baba yake Abdul na vijana wengine wa Dar-es-Salaam kama Mzee bin Sudi (33)na Ibrahim Hamisi kwa kuwataja wachache.

Baadhi ya waasisi hawa Nyerere kawakuta ndani ya TAA Abdul akiwa kiongozi kama Mzee bin Sudi, Ramadhani Mashado Plantan, Schneider Abdillah Plantan na kaka yao Saudtz Thomas Plantan kwa kuwataja wachache.

Historia ya uchaguzi wa mwaka 1953 baina ya Abdul Sykes na Nyerere katika nafasi ya Rais wa TAA nimeieleza mara nyingi.

Sasa hicho alichopindua Nyerere kipi?

Hebu kieleze kifahamike.

Au unakusudia kuuliza imekuwaje Nyerere hakupata kuieleza historia hii muhimu maishani kwake?

Historia hii si ndiyo hii inajadiliwa hapa sasa zaidi ya miaka 10?

Sasa hicho kilichopinduliwa ni kipi?
 
Cmon...
Kitabu kinauzwa Ibn Hazm Media Centre kwenye maduka yao yapo Msikiti wa Mtoro, Manyema, Mtambani na Kichangani bei 10 000.00.

Kipo kwa Kiingereza na Kiswahili.
Kuna kitu ambacho kimetengenezwa Tanzania kutohoji chochote kinachogusa..dini..Mimi ni mkatoliki...ila ni muumini wa kupenda ijua historian...kwakua katika vyote....mda ndo jibu na dawa ya kutenganisha ukweli na uongo...Bado naamini kwa kizazi chetu na kijacho...Tunahitaji sana maandiko tujifunze tulipotoka na tunapoelekea...ntakifuata kitabu mzee
 
Cmoney,
Ahsante sana.
 
Cmon...
Kitabu kinauzwa Ibn Hazm Media Centre kwenye maduka yao yapo Msikiti wa Mtoro, Manyema, Mtambani na Kichangani bei 10 000.00.

Kipo kwa Kiingereza na Kiswahili.
sisi wa mikoani,tuomba mawasiliano tuweze kutumiwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…