kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Hakuna ubishi kuwa Mkude aliwafurahisha wanaSimba kwa miaka 13 mfululizo, aliwatumikia watanzaniaa pia kupitia timu ya Taifa; ni miongoni mwa watanzania muhimu sana. Lakini namna 'THANK YOU" yake ilivyotolewa kwake na Simba ni ushahidi tosha kuwa uongozi wa Simba unamuona Mkude kama mtu punguani anaestahili kwenda kupimwa akili yake kama walivyowahi kusema mbele ya mipaza sauti na camera kuujulisha umma.
Mkude aliachishwa Simba sawa na kama wachezaji wengine ambao hakuonyesha viwango tangu wasajiliwe Simba msimu uliopita tu, yaani alipewa hadhi na uzito sawa na akina Akpan, Kiyombo, Okwa, Okra, Gadiel, na wengine hadi pale baadhi ya wadau kulalamika kwa niaba yake na tetesi za kutakiwa na timu nyingine kubwa simba wakaibuka na mbwembwe na kejeli za kumpa mkude sifa ambazo hawakutaka kumpa hapo awali walipokuwa wanafyeka majina ya wachezaji wa kuondoka Simba.
Kwangu mimi hivyo parade ya heshima wanayotaka kumpa Mkude ni ya kitapeli na yenye nia ovu kwa Mkude. Simba kamwe hawawezi kumpa nafasi ya uongozi Mkude ambae wamejilidhisha kuwa ana utovu wa nidhamu na hana akili nzuri kiasi cha kufika umbali wa kumpeleka akapimwe akili. Maana yake ni kuwa Mkude sio role model kwa wachezaji wa Simba kitabia, hivyo hawezi kuruhusiwa kurudi tena Simba tena kama kiongozi, hivyo kauli ya msemaji wa Simba, Ahmed Ally kuwa Mkude anaruhusiwa kurudi Simba ni uongo, hadaa na kejeli kwa Mkude.
Namshauri Mkude atupe macho na mikono yake juu kumshukuru Mungu kwa kile alichojaliwa kukipata hadi pale alipoambiwa thank you, kisha asonge mbele na mipango yake aliyonayo baada ya kuachwa Simba vinginevyo atajipunguzia heshina, sifa na uwaminifu huko aendako kama atakubali kwenda kuagwa na simba kinafiki ili kumharibia. Gwaride hilo ni la kumharibia sio kumkweza.