Jonas Mkude apimwe akili kama akikubali gwaride la heshima la Simba

Simba kamwe hawawezi kumpa nafasi ya uongozi Mkude ambae wamejilidhisha kuwa ana utovu wa nidhamu na hana akili nzuri kiasi cha kufika umbali wa kumpeleka akapimwe akili.

JONAS MKUDE APIMWE AKILI KAMA AKIKUBALI GWARIDE LA HESHIMA LA SIMBA

Unaishutumu Simba kwa kutaka kumpima akili Mkude, na wakati huo huo unapendekeza apimwe akili. Nadhani kwa contradiction hii unastahili upimwe akili
 
Umeandika fact sana ,kama Mkude anataka kuendelea na mpira basi aachane na hayo Simba wanataka kumfanyia maana itakuwa ni kumroga kama walivyomroga meddy kagere hadi anacheza hovyo
Ye aondoke akatafute malisho huku akiaminiwa na team itakayomsajili kuwa atakuwa mwaminifu kwao na sio kwa Simba labda kama anaenda uarabuni ila kama anabaki bongo aachane na uhuni waliobuni Simba baada ya kugundua kuwa wamemkosea heshima
 
Punguza povu,kapimwe kwanza tuone kama yaliyomo yamo, relax!!
 
Unaishutumu Simba kwa kutaka kumpima akili Mkude, na wakati huo huo unapendekeza apimwe akili. Nadhani kwa contradiction hii unastahili upimwe akili
Ndiyo maana nikasema yeye mwenyewe akapimwe marinda kwanza
 
Haya tuambie wewe unashauri afanye nini?
 
hakika huu ndio ushauri anaopaswa kuutilia manani, kama kweli simba wangekuwa na nia njema basi mechi yao ya mwisho ya ligi ndio ingetumika kumwambia kwaheri father lakini hawakufanya hivyo. Baada ya kusikia malalamiko ya mkuke kupitia wadau mbalimbali ndio wanajifanya kutaka kumuaga kwa heshima. Wamuache tu mtoto wa watu aende anakotakiwa kwa amani bila kumpakaza shombo la kinafiki la usimba. Mkude ataonekana taahila kama atarudi kwaajili ya kuagwa na simba.
 
Haya tuambie wewe unashauri afanye nini?
Amshukuru Mungu kwa kila jambo asisubiri shukrani. Wanaotaka kumuaga walishamtag (label) kuwa ni mtovu wa nidhamu na punguani, halafu mtu anaeitwa Ahmed Ally akatumwa aseme kuwa ataagwa na atapewa nafasi ya kurejea Simba kama kiongozi. NI kiongozi gani mwenye CV ya utovu wa nidhamu na upungufu wa akili? maana yake wanazidi kumfanya punguani.
 
Haya ndiyo mawazo ya wanasimba wote, nani anaenda kumuaga Mkude kutoka rohoni? Tuache unafiki
 
Haya tuambie wewe unashauri afanye nini?
Mfano, mfano, mfano, kama Mkude akisajiliwa Yanga na Yanga wakp pre-season pahala fulani hata kama ni kule malinyi unadhani Yanga watamruhusu aende Simba day akaagwe na simba?
 
Haya ndiyo mawazo ya wanasimba wote, nani anaenda kumuaga Mkude kutoka rohoni? Tuache unafiki
Mbona unawashwa sana na Mkude na Simba ,utanufaika nini na hii fitna unayotengeneza? Uko kama changudoa aliyekopwa,wacha hizo.
 
Uko sahihi kwa lugha nyingine unasema suala la kuachana na mkude lilipaswa kuwa kwenye ratiba ambayo hata yeye mwenyewe angejua kama ilivyokuwa Yanga na Niyonzima
Mechi ya mwisho ingekuwa poa sana kama wanavyofanya wengine,badala yake wanataka kumuaga siku ambayo atakuwa tayari ni mtumishi wa team nyingine anyway kama ni Namungo sawa
 
exactly!! yaani (haswaa!!). Wanadhani kuwa kila mtu ni mjinga. Swala la Mkude kuachwa halikupaswa kuwa siri kwake, club ilipaswa kirafiki kabisa kukaa nae hata miezi 3 nyuma kabla ya ligi kuwa hawana nia ya kuendelea nae kutokana na malengo ya timu ya msimu ujao, hivyo utaratibu wako wa kuondoka utakuwa hivi na vile na pengine akapewa na zawadi ambayo hawapewi wachezaji wengine ambao wanakuja leo na kuondoka leo ili jamaa ajisikikie kuwa haondoki kwa ubaya.
 
Nendeni mkashitaki FIFA,mna kiherehere sana na mambo yasiyowahusu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…