Jonas Mkude atozwa faini ya Sh. Mil 2, atakiwa kurejea kambini

Jonas Mkude atozwa faini ya Sh. Mil 2, atakiwa kurejea kambini

Mbobo

JF-Expert Member
Joined
Jan 13, 2017
Posts
1,392
Reaction score
1,818
Kamati ya Nidhamu ya Klabu ya Simba chini ya mwenyekiti wake Suleiman Kova imetangaza hukumu ya kiungo wa klabu hiyo, Jonas Mkude ambaye alisimamishwa na uongozi kwa makosa ya utovu wa nidhamu.

Kwa mujibu a Kova, haya ndiyo makosa matatu aliyokuwa akituhumiwa kuyafanya, pamoja na hukumu zake.

KOSA LA KWANZA: Kutohudhuria semina elekezi iliyohusisha wachezaji, benchi la ufundi na viongozi. Adhabu yake ni faini ya shilingi milioni moja (1,000,000).

KOSA LA PILI: Kuchelewa kuingia kambini wakati timu ilipokuwa ikijiandaa na mchezo dhidi ya Coastal Union. Adhabu aliyopewa ni karipio kali na faini ya shilingi milioni moja (1,000,000) pamoja na kuwekwa katika kipindi cha uangalizi cha miezi sita.

KOSA LA TATU: Kutoripoti kambini siku ya 26/12/2020 bila ruhusa. Katika tuhuma hizi, kamati haikumkuta na hatia baada ya kamati kutothibitisha pasipo shaka shitaka hilo.

MAAGIZO
Kamati imemtaka Mkude kurejea kambini mara moja kuendelea na mazoezi na asipofanya hivyo atakuwa amefanya tena kosa la utovu wa nidhamu.

Faini aliyotozwa anatakiwa kuilipa ndanI ya mwezi mmoja.

Kamati imemtaka Mkude kuomba radhi kwa maandishi ndani ya saa 24.

Screenshot_2021-01-24_080519~2.jpeg
 
Alaf Et bado aombe msamaha kwa maandish aisee mm swez kubali kabsa
Hao mikia njaa njaa tu znawasumbua
 
Eti kamati ya nidhamu!!!
Mbwembwe za kijinga tu ili kuhalalisha upigaji pesa ili kulipa utitiri wa viongozi waliojaa pale simba.

Naona pia Kova kapata ajira Simba baada ya kustaafu jeshi la Polisi ambapo alitumika kama kondo....
 
Eti kamati ya nidhamu!!!
Mbwembwe za kijinga tu ili kuhalalisha upigaji pesa ili kulipa utitiri wa viongozi waliojaa pale simba.

Naona pia Kova kapata ajira Simba baada ya kustaafu jeshi la Polisi ambapo alitumika kama kondo....
2mil ni hela ndogo sana yaani. Inawalipaje kamati? Hiyo si hela ya mtu mmoja pocket money
 
Ndio maana ww si mkude.
Hoo mm siwez.. hiyo ndio kaz inamuweka hapa mjini.
Lazima uipambania au urud kitaa
N Sawa Lakin kama alishakir na Fain zote hzo bado naskia kapewa karipio kali aisee
 
wabongo bwana angesamehewa bila masharti ungesikia simba wakubali yaishe wamrudisha mkude kundini ... mara mkude mkubwa kuliko simba... maana ndo ulikuwa utabiri wa wabongo

sasa hv ohh faini kubwa alishaomba msamaha kwa nini apewe karipio kali huo uonevu..

mwingine wanasema simba wamenywea faini ndogo

sasa jaman mnatakaje...
 
Ningekuwa Mimi huyo Mkude ningerudi nikiwa na plan B ya kuondoka hapo. Kwanza ni mchezaji mzuri ananunulika. Tena ningehamia Yanga
 
N Sawa Lakin kama alishakir na Fain zote hzo bado naskia kapewa karipio kali aisee
Mbona ni mambo ya kawaida. Haijalish kapeqa karipio la blue au jekundu.
Cha msingi ni ame retain kibarua chake.
 
Alaf Et bado aombe msamaha kwa maandish aisee mm swez kubali kabsa
Hao mikia njaa njaa tu znawasumbua
kila club ina utaratibu wake, huwezi kuingilia maamuzi ya club fulani kwa kuwa uhusiki na huijui katiba yao.
ingekuwa busara zaidi kama usingecomment kabisa
 
Back
Top Bottom