Jonas Mkude atozwa faini ya Sh. Mil 2, atakiwa kurejea kambini

Jonas Mkude atozwa faini ya Sh. Mil 2, atakiwa kurejea kambini

Kamati ya Nidhamu ya Klabu ya Simba chini ya mwenyekiti wake Suleiman Kova imetangaza hukumu ya kiungo wa klabu hiyo, Jonas Mkude ambaye alisimamishwa na uongozi kwa makosa ya utovu wa nidhamu.

Kwa mujibu a Kova, haya ndiyo makosa matatu aliyokuwa akituhumiwa kuyafanya, pamoja na hukumu zake.

KOSA LA KWANZA: Kutohudhuria semina elekezi iliyohusisha wachezaji, benchi la ufundi na viongozi. Adhabu yake ni faini ya shilingi milioni moja (1,000,000).

KOSA LA PILI: Kuchelewa kuingia kambini wakati timu ilipokuwa ikijiandaa na mchezo dhidi ya Coastal Union. Adhabu aliyopewa ni karipio kali na faini ya shilingi milioni moja (1,000,000) pamoja na kuwekwa katika kipindi cha uangalizi cha miezi sita.

KOSA LA TATU: Kutoripoti kambini siku ya 26/12/2020 bila ruhusa. Katika tuhuma hizi, kamati haikumkuta na hatia baada ya kamati kutothibitisha pasipo shaka shitaka hilo.

MAAGIZO
Kamati imemtaka Mkude kurejea kambini mara moja kuendelea na mazoezi na asipofanya hivyo atakuwa amefanya tena kosa la utovu wa nidhamu.

Faini aliyotozwa anatakiwa kuilipa ndanI ya mwezi mmoja.

Kamati imemtaka Mkude kuomba radhi kwa maandishi ndani ya saa 24.

View attachment 1684629
Na hiyo faini analipa boss lady.
 
Aende yanga kama atapata pesa kama ya Simba, sasa hivi Simba wameshajiandaa kuishi bila Mkude ndio maana unaona wanasajili viungo wakabaji wengi
Au Azam. Ila Yanga ni muda tu watarudi ulingoni. Mimi ni Simba lakini. Shabiki Kindakindaki
 
Ujuaji wa Mkude umemponza kukosa milioni 250 walizopewa Simba baada ya kuwatoa platnum, pia amekosa kuitwa timu ya taifa inayoshiriki chan sasa akae ajitafakari kqma anafikiri alikuwa anaikomoa Simba alikuwa anajikomoa mwenyewe
 
Back
Top Bottom